Mbingu
Kwa mbingu kama uwazi juu tunayoona juu ya uso wa ardhi penye mawingu, jua na nyota tazama anga
Mbingu ni upeo wa Mungu au miungu katika mafundisho ya dini nyingi. Mara nyingi humaanisha pia upeo wa kiroho ambako nafsi za wafu hufikia baada ya kifo.
Watu walioishi zamani wakitegemea macho yao pekee waliona mara nyingi ya kwamba mbinguni ni juu yetu na tukitazama anga tunaona mwanzo wa mbingu kama mahali pa Mungu.
Lakini tangu kale watu wengine waliona ya kwamba mbingu si mahali maalumu bali zaidi hali au upeo ambao ni tofauti kuliko mahali popote tunapojua au tunapoweza kutambua.
Anga na mbingu [hariri]
Katika lugha ya kila siku maneno "anga" na "mbingu" mara nyingi yanatumiwa kwa maana moja: "Mawingu yanatembea angani - mawingu yanatembea mbinguni". Lakini mbingu huwa na maana ya ziada yaani ya kidini kwa kutaja pia upeo wa Mungu au hali inayopita maarifa ya duniani: "hapa ninajisikia kama mbinguni" ni tofauti sana na "hapa najisikia angani". Katika wikipedia hii tunatumia neno "mbingu" zaidi kwa maana ya kidini.
| Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |