Kitabu cha Danieli
Kitabu cha Danieli ni kimojawapo kati ya vitabu vya Tanakh yaani Biblia ya Kiebrania ambamo kimo katika kundi la mwisho (Ketuvim). Awali kiliandikwa katika lugha ya Kiebrania na Kiaramu.
Wakristo wengi wanafuata tafsiri ya Septuaginta yenye nyongeza mbalimbali kwa lugha ya Kigiriki na kukipanga kati ya vitabu vya manabii baada ya Kitabu cha Ezekieli katika Biblia ya Kikristo.
Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.
Yaliyomo |
[hariri] Maana ya jina
Tafsiri ya kawaida ja jina la mhusika mkuu, Danieli mwenye hekima ni Mungu ni hakimu wangu.
[hariri] Habari za Danieli
Kadiri ya kitabu, Danieli alipokuwa kijana alipelekwa uhamishoni Babuloni, ambako hekima yake ya pekee ilimvutia mfalme Nebukadneza II na kumpatia cheo katika ikulu.
Sifa yake ilimwezesha kuendelea na cheo chake hata baada ya mji huo kutekwa na Wamedi na Waajemi (539 a.C.), ambapo alipendwa hasa na mfalme Dario ingawa alikataa amri zilizokwenda kinyume cha imani na maadili ya Torati ya taifa lake, Israeli.
Mtu mwenye hekima aitwaye Danieli alitajwa mapema hata nje ya Biblia katika eneo la Mashariki ya Kati.
Wataalamu wengi wa Biblia siku hizi hawakubali habari hizi kuwa za kihistoria kutokana na makosa mengi kuhusu watu na matukio.
Vilevile hawakubali matabiri yake kuwa za kinabii, kwa maana kitabu kinaonekana kimeandikwa na watu mbalimbali na nyakati mbalimbali hadi kikakamilika katika karne ya 2 K.K. kilipokusudiwa kutegemeza Wayahudi washike kama yeye msimamo katika dhuluma za mfalme Antioko Epifane zilizowakabili kama vinavyoeleza vitabu vya Wamakabayo.
Kwa sababu hiyo mtindo wake ni wa kiapokaliptiko, kama vitabu vingi vya wakati huo, kuanzia sehemu za Ezekieli hadi kitabu cha Ufunuo
[hariri] Mgawanyo wa kitabu
Sura sita za kwanza zinasimulia hadithi za maisha ya Danieli.
Sura sita zinazofuata zinaleta njozi nyingi za usiku.
Sura za 13 na 14 ni sehemu za nyongeza kati ya Deuterokanoni.
[hariri] Ujumbe
Kwa Wakristo ni muhimu hasa maneno ya kitabu juu ya Mwana wa Adamu, jina la mtu wa kimbingu lililotumiwa sana na Yesu ili kujitambulisha.
Vilevile ni muhimu fundisho lake la wazi kuhusu ufufuko wa watu wote na hali mbili tofauti za milele zitakazokana na hukumu juu yao. Ni hatua ya maana katika maendeleo ya ufunuo kuhusu vikomo vya binadamu
[hariri] Viungo vya Nje
Kitabu cha Danieli katika tafsiri ya Kiswahili ya sehemu za Kiebrania na Kiaramu (Union Version)
Mwanzo Kutoka Walawi Hesabu Kumbukumbu Yoshua Waamuzi Ruthu Samueli I Samueli II Wafalme I Wafalme II Mambo ya Nyakati I Mambo ya Nyakati II Ezra Nehemia TobitiDK YudithiDK Esta Wamakabayo IDK Wamakabayo IIDK Yobu Zaburi Methali Mhubiri Hekima DK SiraDK Wimbo Bora Isaya Yeremia Maombolezo BarukuDK Ezekieli Danieli Hosea Yoeli Amosi Obadia Yona Mika Nahumu Habakuki Sefania Hagai Zekaria Malaki - Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.