Kitabu cha Habakuki
Habakuki ni jina la nabii wa Israeli ya Kale na pia la kitabu kinacholeta habari zake katika Tanakh (yaani Biblia ya Kiebrania), na kwa hiyo pia katika Agano la Kale, sehemu ya kwanza ya Biblia ya Kikristo.
[hariri] Muda na mada
Wakati alipofanya kazi nabii Yeremia aliishi pia Habakuki (600 hivi K.K.), aliyeandika kitabu kifupi ambamo alithubutu kumuuliza Mungu kwa nini anaadhibu Israeli vikali kwa mikono ya watu wabaya kuliko wao.
Jibu ni kwamba Mungu ana njia zake ambazo anaandaa ushindi wa haki: hivyo mwadilifu ataishi kwa imani yake (1:12-2:4). Usemi huo ukaja kutumika sana katika Agano Jipya. Mtume Paulo ameufanya msingi wa msimamo wake kuwa wokovu unapatikana kwa imani, si kwa kujitahidi kutekeleza masharti yote ya Torati.
[hariri] Ufafanuzi
Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.
[hariri] Viungo vya Nje
Kitabu cha Habakuki katika tafsiri ya Kiswahili (Union Version)
Mwanzo Kutoka Walawi Hesabu Kumbukumbu Yoshua Waamuzi Ruthu Samueli I Samueli II Wafalme I Wafalme II Mambo ya Nyakati I Mambo ya Nyakati II Ezra Nehemia TobitiDK YudithiDK Esta Wamakabayo IDK Wamakabayo IIDK Yobu Zaburi Methali Mhubiri Hekima DK SiraDK Wimbo Bora Isaya Yeremia Maombolezo BarukuDK Ezekieli Danieli Hosea Yoeli Amosi Obadia Yona Mika Nahumu Habakuki Sefania Hagai Zekaria Malaki - Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.