Donatello

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Sanamu ya Donatello mjini Firenze
Daudi, kichwa na mabega

Donato di Niccolò di Betto Bardi (*1386 hadi 13 Desemba, 1466) huitwa kwa kawaida Donatello (Donato mdogo) alikuwa msanii wa zama ya mwamko nchini Italia. Alikuwa mwenyeji wa mji wa Firenze akawa mchongaji mashuhuri wa wakati wake.

Donatello alizaliwa Firenza kama mtoto wa fundi wa kuchanua sufi Niccolò di Betto Bardi. Mnamo 1401 alianza kazi kama msaidizi wa mchongaji na fundi shahabu Lorenzo Ghiberti. Anasemekana alisafiri Roma na kutazama sanamu za Waroma wa Kale.

Tangu 1407 alionekana kama fundi na mchongaji wa kujitegemea aliyepewa kazi ya kupamba makanisa na majumba ya matajiri. Alionyesha ya kwamba alijifunza mwengi kutoka sanaa ya Waroma wa Kale hivyo alikuwa kiongozi wa harakati ya mwamko wa sanaa ya kale katika Italia iliyoathiri sanaa kote Ulaya.

Donatello alitumia ubao, mwamba na metali kwa kazi zake. Kati ya sanamu zake zilizokuwa mashuri sana ni Daudi kama mchungaji kijana na Maria Magdalene.

[hariri] Viungo vya Nje

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


WikiLettreMini.svg Makala hiyo kuhusu "Donatello" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri".

Ikiwepo makala kuhusu Donatello kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili.