Mtakatifu Marko

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mtakatifu Marko

Mtakatifu Marko (kwa Kilatini Mārcus; kwa Kigiriki Μᾶρκος) aliishi katika karne ya 1 BK. Alikuwa Myahudi wa Yerusalemu aliyeongokea mapema Ukristo pamoja na Maria mama yake. Kanisa la kwanza lilikuwa linakusanyika nyumbani mwao.

Alifanya kazi na mitume Paulo na Barnaba katika kuhubiri Injili huko Kupro na Uturuki.

Baadaye alikuwa na Mtume Petro na Paulo katika mji wa Roma hadi walipouawa na serikali ya Kaisari Nero (64-67).

Ndipo alipoandika Injili ya kwanza, iliyofuatwa na Mtume Mathayo na Mwinjili Luka, ingawa katika orodha za Biblia inashika nafasi ya pili.

Kadiri ya mapokeo alifariki wakati akifanya kazi hiyo huko Alexandria nchini Misri.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Bible.malmesbury.arp.jpg Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mtakatifu Marko kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.