Yosefu (mume wa Maria)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Arusi ya Bikira Maria ya Perugino

Yosefu, kadiri ya Injili, alikuwa mume wa Bikira Maria na baba mlishi wa Yesu Kristo ambao pamoja naye waliunda Familia takatifu.

Jina linatokana na Kiebrania Yosef.

[hariri] Maisha

Katika Injili ya Mathayo 13:5) anatajwa kama "fundi", (kwa Kigiriki téktón). Lakini inasema pia (sawa na Injili ya Luka) kuwa alitoka katika ukoo wa kifalme wa Daudi.

Injili na imani ya Kikristo zinasisitiza kuwa baba halisi wa Yesu alikuwa Mungu mwenyewe: Maria alimchukua mimba kwa muujiza uliosababishwa na Roho Mtakatifu.

Ndoto ya Mt. Yosefu, mchoro wa Josè Luzan

Yosefu, kisha kujulishwa juu ya mimba hiyo, alikubali kumchukua mchumba wake nyumbani na kumtambua mwanae kuwa ni wa kwake ingawa hakuwahi kujamiana naye. Hivyo alitunza heshima ya mama na mtoto na kuwahakikishia ulinzi katika jamii inayojali wanaume.

Miezi baadaye familia yake ilikwenda Bethlehemu kwa ajili ya sensa, na ndipo Yesu alipozaliwa pangoni na kulazwa horini.

Wakati huo Yosefu alishuhudia ujio wa wachungaji waliokuja kumuabudu mtoto kadiri ya tangazo la malaika waliowatokea.

Kadiri ya Torati ya Musa, siku nane baada ya mtoto kuzaliwa, Yosefu alimpa mtoto jina wakati wa kutahiriwa, na siku arubaini baadaye alimpeleka hekaluni Yerusalemu ili kumtolea Mungu kama mtoto wa kiume wa kwanza. Ndipo wazee Simeoni na Anna binti Fanueli walipotoa utabiri juu ya Yesu.

Baada ya mamajusi kuwatembelea Bethehemu, wanafamilia walikimbilia Misri ili kukwepa dhuluma ya mfalme Herode Mkuu aliyetaka kumuua mtoto.

Kisha wakarudi Nazareti (Galilaya) ambapo Yesu alikua vizuri chini ya wazee wake.

Yesu alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, wote watatu walikwenda kuhiji Yerusalemu kwa Pasaka. Wakati wa kurudi, mtoto alibaki mjini akapatikana tena siku ya tatu akiwa hekaluni kati ya walimu wa sheria, akitokeza hekima yake. Alipoulizwa na Maria kuhusu mwenendo wake, mtoto alionyesha kujitambua si mwana wa Yosefu, bali wa Mungu.

Baada ya taarifa hiyo, hakuna tena habari juu ya Yosefu, hivi kwamba wengi wanajiuliza kuhusu kifo chake na kuhisi kilikuwa kimeshatukia Yesu alipoanza utume wake.

[hariri] Heshima yake

Anaheshimiwa kama mtakatifu na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi. Heshima hiyo ilizidi kukua hasa magharibi kadiri ulivyozingatiwa ubinadamu wa Yesu.

Vifaa binafsi
Maeneo ya wiki

Vibadala
Vitendo
Urambazaji
Vifaa
Lugha zingine