Hija

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Wayahudi wakisali kwenye Ukuta wa Maombolezo, Yerusalemu.
Hija ya Waislamu kwenye Masjid al-Haram, Maka, mwaka 2008.

Hija (kutoka Kiarabu حج, Ḥaǧǧ) ni safari inayofanyika kwa sababu ya dini, ikilenga patakatifu fulani.

Kwa maana ya kiroho, maisha yote ni safari ya kumuelekea Mungu au uzima wa milele n.k.

Desturi ya kuhiji iko katika dini mbalimbali.

Kiasili neno "hija" katika Kiswahili lilimaanisha tu safari ya Waislamu kwenda Makka kwa sababu katika utamaduni wa Waswahili hili lilikuwa safari ya kidini pekee yenye jina maalumu.

Lakini Wakristo wamepokea neno hili pia kwa safari zao za kiroho na siku hizi linatumiwa kwa kutaja safari za aina hii kwa jumla kati ya dini zote.

Icon-religion.png Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Hija kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.