Bikira Maria wa Mateso

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mchoro wa Carlo Dolci, Mater Dolorosa, 1650 hivi.

Bikira Maria wa Mateso ni jina mojawapo linalotumika kumheshimu mama wa Yesu kama mshiriki wa mateso na kifo cha Mwanae msalabani.

Liturujia ya Kanisa la Kilatini inaadhimisha kumbukumbu yake tarehe 15 Septemba, siku inayofuata sikukuu ya Kutukuka kwa Msalaba[1].

Ndivyo ilivyopangwa na Papa Pius X kwa dunia nzima mwaka 1913, baada ya heshima hiyo kuenea sana katika ya Wakatoliki kuanzia karne ya 11.

Msingi wake ni hasa habari za Injili ya Luka (2:34-35,41-51; 23:27-31,55-56) na ya Yohane (19:25-27), lakini pia ile ya Mathayo (2:13) kuhusu mtoto Yesu kudhulumiwa na mfalme Herode Mkuu .

Katika liturujia ya Neno, Misa ya siku hiyo ina sekwensya ya pekee, ambayo kwa Kilatini inaitwa "Stabat Mater" ("Mama alisimama"), ambayo ndiyo maneno ya kwanza ya shairi hilo lenye muziki wa huzuni lakini mtamu.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Martyrologium Romanum
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bikira Maria wa Mateso kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.