Sikukuu
Mandhari
Sikukuu ni siku maalumu ya kukumbuka, kusheherekea au kufurahia jambo fulani.
Kuna sikukuu za binafsi na sikuu za umma. Sikukuu ya umma mara nyingi huwekwa wakfu kisheria maana yake si siku ya kazi bali ya mapumziko.
Kati ya sikuu za umma kuna sikukuu za kidini na sikukuu za kiserikali.
Kati ya sikukuu za binafsi kuna siku za kukumbuka matukio ya pekee kama tarehe ya kuzaliwa, kumbukumbu ya siku ya kufunga ndoa na mengine.
Sikukuu za kidini
[hariri | hariri chanzo]Sikukuu za Ukristo
[hariri | hariri chanzo]- Majilio (Ujio wa Yesu)
- Krismasi (Kuzaliwa kwake Yesu)
- Epifania (Bwana kuwatokea mataifa)
- Ijumaa Kuu (Kifo cha Yesu)
- Pasaka (Ufufuko wa Yesu)
- Kupaa Bwana (Yesu kuingia mbinguni)
- Pentekoste (Roho Mtakatifu kulishukia Kanisa)
- Watakatifu wote
Sikukuu za Uislamu
[hariri | hariri chanzo]Sikukuu za Kiislamu hufuata kalenda ya Kiislamu. Kwa hiyo tarehe za sikukuu hizi katika kalenda ya Gregori hubadilikabadilika.
- Ashurah tar. 1-10 muharram
- Idd-ul-Fitr mwisho wa ramadan
- Idd-ul-Adha tar. 10 dhu l-hija
- Mawlidi-ar-Rasul tar. 10 rabi' al-auwal
Sikukuu za Uhindu
[hariri | hariri chanzo]- Diwali pia "Deepavali" - mwezi wa Oktoba au Novemba
Sikukuu za Serikali
[hariri | hariri chanzo]Hutofautiana kati ya nchi na nchi lakini mara nyingi huwa na: