Pasaka

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

GrunewaldR.jpg
Mwaka wa liturujia
Magharibi
Mashariki
Israel 5 010.jpg Via Dolorosa- Walk in Jerusalem, with Jesus Christ-Actor and Press.jpg
Easter eggs - straw decoration.jpg

Pasaka ni jina la sikukuu muhimu katika dini za Uyahudi na Ukristo. Jina la Pasaka limetokana na neno la Kiebrania "פסח" (tamka: pasakh).

  • Pasaka ya Kikristo ni sikukuu ya kukumbuka kufufuka kwake Yesu Kristo siku ya tatu baada ya kusulibiwa kwake. Inahesabiwa kuwa sikukuu muhimu kabisa katika Ukristo.

Taarifa za Agano Jipya zinatoa habari ya kuwa kifo na kufufuka kwa Yesu yametokea wakati wa sikukuu ya Pasaka ya Kiyahudi. Kwa hiyo jina la sikukuu hiyo imeendelea kutumikwa kwa ajili ya sherehe ya kikristo.

[hariri] Majina ya Pasaka ya Kiyahudi na Pasaka ya Kikristo katika lugha mbalimbali

Katika lugha nyingi asili hii bado inaonekana ingawa mara nyingi umbo la neno ni tofauti kidogo. Jina la sikukuu ya Kiyahudi linapatikana kwa umbo mbalimbali. Siku hizi mara nyingi umbo la neno la Kiebrania limetumika lakini desturi katika lugha hizo inaonyesha pia umbo linalofanana zaidi na neno kwa ajili ya sherehe ya Kikristo.

Lugha Jina la Pasaka ya Kiyahudi Jina la Pasaka ya Kikristo
Kifaransa Pessah Paque; Les Paques
Kihispania pascua pascua
Kiitalia Pasqua ebraica; Pesach; Pesah Pasqua
Kipoland Pesach Wielkanoc; Pascha
Kirusi Пасха; Песах (pas-kha; pesakh) Пасха (pas-kha)
Kigiriki Πάσχα (pas-kha) Πάσχα (pas-kha)
Kidenmark Pesach Påske
Kinorwei Pesah Påske
Kiswidi Pesach;Påsk Påsk
Kiholanzi Pesach Pasen
Kijerumani Passah Ostern
Kiingereza Passover Easter
Kiajemi پسح

پاک

WikiLettreMini.svg Makala hiyo kuhusu "Pasaka" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri".

Ikiwepo makala kuhusu Pasaka kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili.

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu: