Agano Jipya

Kutoka Wikipedia

Agano Jipya

Agano Jipya ni sehemu ya pili ya Biblia ya kikristo yenye vitabu 27. Yaleta habari za Yesu Kristo, mitume yake na chanzo cha kanisa la Kikristo.

Yaliyomo

[hariri] Vitabu vya Agano Jipya

(Kwa mabano: kifupi cha kawaida kwa kutaja kitabu hiki)

[hariri] Vitabu vya kihistoria

Injili nne zasimulia habari za Yesu.

Historia ya chanzo cha kanisa iko katika

[hariri] Nyaraka

[hariri] Nyaraka za Paulo

Kuna maandiko 13 kati ya nyaraka yanayomtaja Mtume Paulo kama mwandishi. Wataalamu wa leo hutofautiana kama kweli nyaraka hizi zote zimeandikwa na Paulo mwenyewe. Kwa jumla saba zimetambuliwa na karibu wataalamu wote kuwa ni maandiko yake. Kuhusu mengine kuna maswali kwa sababu mbalimbali (kwa mfano tofauti za lugha, mkazo tofauti ya mafundisho) na wataalamu wengine hudai ya kuwa labda zimeandikwa na wanafunzi wake au na mwandishi kwa niaba ya Paulo.

[hariri] Waebrania

  • Waraka kwa Waebrania (Ebr.) una tabia ya pekee; tangu zamani ulihesabiwa kuwa waraka wa Paulo lakini ndani yake jina la Paulo halitajwi.

[hariri] Nyaraka katoliki

Jina "katoliki" halimaanisha dhehebu la Kiroma-katoliki lakini maana asilia ya neno la kigriki katoliki ambayo ni "kwa watu wote". Maana yake hazilengi ushirika maalumu au kikundi fulani ndeani ya Ukristo lakini ziliandikwa kwa wakristo wote kwa jumla. Nyaraka hizi zote ziliandikwa katika jina la mtume fulani wa Yesu au Mkristo mwingine wa kanisa la kwanza.

[hariri] Kitabu cha kinabii

[hariri] Viungo vya Nje

Toleo la Agano Jipya kwa Kiswahili


Image:WikiLettreMini.png Makala hiyo kuhusu "Agano Jipya" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri".

Ikiwepo makala kuhusu Agano Jipya kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili.

Vifaa binafsi