Waraka wa pili kwa Wathesaloniki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Agano Jipya


Waraka wa pili kwa Wathesalonike ni skati ya vitabu 27 vya Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo.

Ni barua ya Paulo wa Tarso kwa ushirika wa Kikristo katika mji wa Thesalonike (Ugiriki wa Kale).

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

[hariri] Mazingira

Miezi michache baada ya Mtume Paulo kuwaandikia Wakristo wachanga wa Thesalonike barua tulivu, akarudia kuwaandikia kutokana na taarifa nyingine zilizomtia tena wasiwasi.

Akawafafanulia zaidi ujio wa Bwana na dalili zake, akiwahimiza hasa kufanya kazi kwa bidii badala ya kuiacha kwa kisingizio cha kwamba, eti Kristo amesharudi (2Thes 2:1-15; 3:6-15).

[hariri] Mpangilio

Mpangilio wa barua hizo ni uleule wa barua zitakazofuata: baada ya salamu na shukrani kwa Mungu, yanafuata mafundisho ya imani, halafu maadili, na hatimaye salamu nyingine.

Vifaa binafsi
Maeneo ya wiki

Vibadala
Vitendo
Urambazaji
Vifaa
Lugha zingine