Waraka wa kwanza wa Petro

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Agano Jipya


Barua ya kwanza ya Petro ni kati ya vitabu 27 vinavyounda Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

[hariri] Mazingira

Mtume Paulo alipokaribia kumaliza kazi yake, wengine kati ya mitume na wanafunzi wao walianza kuandika kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu.

Mmojawao ni Petro, kwa msaada wa Sila, akiwa Roma karibu na kuuawa (mwaka 64 hivi).

Baada ya kufanya utume Antiokia, aliweza kwa urahisi kutembelea mikoa ya Uturuki Kaskazini wa leo.

Wakristo wa huko ndio walioandikiwa barua hii yenye mafundisho na ibada kuhusu ubatizo na Pasaka.

Pamoja na hayo walihimizwa wasiogope maneno ya watu wengine wasiopendezwa na uongofu wao: hali ngumu ni fursa ya kulingana zaidi na Yesu mpole na mteswa (1Pet 1:1-12; 2:19-25; 3:13-5:14).


[hariri] Kiungo cha nje

  • [1] Agano Jipya kwa lugha ya Kiswahili