Waraka kwa Tito
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Barua kwa Tito ni kimojawapo kati ya vitabu 27 vya Agano Jipya katika Biblia ya Ukristo.
Pamoja na barua mbili kwa Timotheo inaunda kundi la Nyaraka za Kichungaji. Mada za hizo zote ni mafundisho sahihi ya imani na uadilifu wa matendo yanayofuatana nayo.
Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.
[hariri] Mwandishi
Mwandishi wake ni Mtume Paulo mwishoni mwa maisha yake.
[hariri] Mlengwa
Mlengwa ni mmojawapo wa wanafunzi wake, ambao aliwashirikisha mamlaka yake wakawa waandamizi wake ka maaskofu wa kwanza.
Awali Tito alikuwa Mpagani (Wagalatia 2:1-3, 2 Wakorintho 8:23).
[hariri] Kiungo cha nje
- [1] Agano Jipya kwa lugha ya Kiswahili