Waraka kwa Waroma

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Agano Jipya


Waraka kwa Waroma ni sehemu ya Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo. Andiko hili ni barua ya Paulo wa Tarso kwa ushirika wa Kikristo katika mji mkuu wa Dola la Roma.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Kati ya maandiko matakatifu ya Agano Jipya na ya Biblia kwa jumla, barua ya Mtume Paulo kwa Wakristo wa Roma ina umuhimu wa pekee uliokusudiwa naye mwenyewe.

Ingawa yeye alikaa Efeso miaka mitatu, moyo wake wa kimisionari haukutulia kwa sababu alikumbuka alivyotabiriwa atafanya kazi hata mbali zaidi.

Ndiyo maana alitaka kwenda Ulaya magharibi, yaani Roma na halafu Hispania, nchi iliyohesabika kuwa mwisho wa dunia.

Ila kabla ya kwenda huko alipanga kuleta mchango kwa Wakristo wa Yerusalemu.

Basi, mwishoni mwa miezi mitatu aliyokaa Korintho (Mdo 20:2-3) yaani mwanzoni mwa mwaka 58, Paulo aliwaandikia Wakristo wa Roma ili kuandaa utume atakaoufanya katika jiji hilo ambapo Ukristo uliingia toka mwanzo kabisa, ukiletwa na baadhi ya Wayahudi wengi walioishi huko ambao walibatizwa Yerusalemu kwenye Pentekoste ya mwaka 30.

Wayahudi walipofukuzwa mwaka 49, Wakristo wa mataifa mengine wakabaki ndio wengi, nao ndio walioandikiwa barua hiyo miaka 9 baadaye.

Mtume Paulo akijua umuhimu wa Roma, mji mkuu wa ulimwengu wa zamani hizo, aliwaandikia Wakristo wa huko barua ndefu tena nzito kuliko zote.

Ingawa haina mafundisho yote ya Paulo, imechangia teolojia ya Kikristo kwa kiasi kikubwa, hasa upande wa magharibi.

Kwa namna ya pekee inajibu maswali kuhusu wokovu: unapatikana kwa njia gani? Kwa nini Wayahudi wengi walishindwa kumuamini Yesu ili kuupata? Kwa nini mataifa yameupokea badala yao? Aliyepata wokovu anaishi vipi? Je, Wayahudi wametupwa moja kwa moja?

Ndiyo sehemu kuu ya barua (Rom 1:16-32; 2:1-29; 3:9-20; 3:21-31; 4:1-8; 4:23-25; 5:1-21; 6:1-14; 7:7-25; 8:1-39; 9:1-5; 11:1-36).

Kabla yake kuna salamu (1:1-8) na shukrani.

Sehemu ya pili ni mawaidha mbalimbali Rom 12:1-2,9-21; 13:8-14) yakifuatwa na taarifa na salamu.


[hariri] Kiungo cha nje

  • [1] Agano Jipya kwa lugha ya Kiswahili
Vifaa binafsi
Maeneo ya wiki

Vibadala
Vitendo
Urambazaji
Vifaa
Lugha zingine