Waraka kwa Waefeso

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Maandishi ya Kijerumani ya maneno kutoka waraka huu, "Bwana mmoja, imani moja, Ubatizo mmoja" (Ef 4:5).
Agano Jipya

Barua kwa Waefeso ni kati ya vitabu 27 vya Agano Jipya ambalo pamoja na Agano la Kale linaunda Biblia ya Kikristo.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Mazingira[hariri | hariri chanzo]

Mtume Paulo aliweza kuandika barua hii akiwa kifungoni Roma kati ya miaka 61 na 63 ili isomwe katika makanisa yote ya mkoa wa Asia Ndogo, wenye makao makuu mjini Efeso.

Mada[hariri | hariri chanzo]

Mafundisho yake yanalingana na yale ya barua kwa Wakolosai ila yamechimbwa zaidi, kiasi kwamba barua hii inaonekana kuwa kilele cha teolojia ya Paulo.

Pamoja na kuchambua fumbo la wokovu katika Yesu Kristo, inachambua hasa fumbo la Kanisa kama mwili wa Kristo ambamo kichwa kinaeneza wokovu ulimwenguni kote.

Kwa msingi huo inasisitiza na kudai umoja kamili kati ya waamini (Ef 1:1-2; 1:17-23; 2:11-22; 3:1-21; 4:1-16).

== Viungo vya nje ==

Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:

Tafsiri ya Kiswahili[hariri | hariri chanzo]

  • [1] Agano Jipya kwa lugha ya Kiswahili

Vingine[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya Agano Jipya bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Waraka kwa Waefeso kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.