Waraka wa kwanza kwa Wathesaloniki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Agano Jipya

Waraka wa kwanza kwa Wathesalonike ni sehemu ya Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo. Ni barua iliyoandikwa na Paulo wa Tarso kwa Wakristo wa mji wa Thesaloniki katika Ugiriki ya Kale.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Yaliyomo

[hariri] Muda wa uandishi

Barua hiyo ni andiko la kwanza la Agano Jipya katika Biblia kwa kuwa ni wa mwaka 51 hivi.

[hariri] Mazingira

Baada ya Sila na Timotheo kufika Korintho toka Thesaloniki, walimpa Mtume Paulo ripoti kuhusu hali ya Kanisa la kule na kumuondolea wasiwasi: dhuluma zilikuwa zikiendelea lakini Wakristo wapya ni imara.

Kwa furaha Paulo akawaandikia barua hiyo tuliyonayo mpaka leo ambayo haina mafundisho mazito isipokuwa kuhusu mambo ya mwisho (hali ya marehemu na ujio wa pili wa Bwana).

Ni barua tulivu na ya kirafiki, ingawa inatoa maonyo upande wa maadili (1Thes 1:1-3:13; 4:13-17; 5:1-11; 5:16-28).

[hariri] Mpangilio

Mpangilio wa barua ni uleule wa zile zitakazofuata: baada ya salamu na shukrani kwa Mungu, yanafuata mafundisho ya imani, halafu maadili, na hatimaye salamu nyingine.


[hariri] Kiungo cha nje

  • [1] Agano Jipya kwa lugha ya Kiswahili

]