Waraka wa pili kwa Wakorintho
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Waraka wa pili kwa Wakorintho ni sehemu ya Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo.
Katika Biblia, Agano Jipya linatunza barua mbili za Mtume Paulo kwa Wakristo mjini Korintho (Ugiriki).
Mdo 19:21-20:1 inasimulia alivyohama Efeso kutokana na matatizo kuzidi, akaelekea Makedonia na Ugiriki.
Toka huko alipata nafasi ya kuhubiri huko Iliriko, yaani Albania ya leo kwenda kaskazini (Rom 15:19).
Wakati huo alipata habari mbaya kuhusu Wakorintho, akawaandikia tena na tena kabla hajawaendea kwa mara ya tatu.
Labda kwa kuwa ni mshono wa barua hizo mbalimbali, mpangilio wa 2Kor haueleweki, ingawa ina salamu na shukrani mwanzoni, na salamu nyingine mwishoni kama kawaida.
Katikati mada kuu ni tatu: kujitetea, mchango na mashambulizi dhidi ya wapinzani.
Barua hiyo inatusaidia hasa kumjua Paulo mwenyewe (2Kor 11:1-12:13).
[hariri] Kiungo cha nje
- [1] Agano Jipya kwa lugha ya Kiswahili

