Sikusare

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tarehe na saa za UTC
za sikusare na solistasi duniani[1][2]
Tukio Sikusare Solistasi Sikusare Solistasi
Mwezi Machi Juni Septemba Disemba
Mwaka
Siku Saa Siku Saa Siku Saa Siku Saa
2018 20 16:15 21 10:07 23 01:54 21 22:23
2019 20 21:58 21 15:54 23 07:50 22 04:19
2020 20 03:50 20 21:44 22 13:31 21 10:02
2021 20 09:37 21 03:32 22 19:21 21 15:59
2022 20 15:33 21 09:14 23 01:04 21 21:48
2023 20 21:24 21 14:58 23 06:50 22 03:27
2024 20 03:07 20 20:51 22 12:44 21 09:20
Mwangaza wa Dunia na Jua kwenye ikweta

Sikusare (pia: siku mlingano au ikwinoksi kutoka Kilatini na Kiingereza equinox; [3]) ni siku ambako urefu wa mchana na usiku ni sawa kote duniani.

Hii inatokea mara mbili kila mwaka, mara ya kwanza mnamo 21 Machi (sikusare machipuo) na 23 Septemba (sikusare otomnia).

Katika kanda karibu na ikweta hazionekani kwa urahisi lakini kwenye nusutufe za dunia upande wa kusini na kaskazini wa ikweta zimetambuliwa tangu karne nyingi na zimekuwa siku muhimu kwa makadirio ya kalenda mbalimbali.

Kwa kawaida kuna tofauti kati ya urefu wa mchana na usiku isipokuwa karibu na ikweta. Karibu na ncha za dunia muda wa usiku na mchana unaweza kuwa mrefu hadi karibu nusu mwaka lakini kwa kawaida kuna majira ya mchana mrefu na usiku mrefu zinazobadilishana polepole.

Kuanzia usawa wa mchana na usiku kwenye sikusare muda wa mchana unarefuka au kupungua polepole kati ya kufikia ama siku ya mchana mrefu au usiku mrefu unaotokea katikati ya sikusare mbili za mwaka halafu mwendo hutokea kinyume hadi kufikia sikusare tena.

Mwendo huo unatokea kinyume kwenye nusutufe mbili za dunia yaani wakati mchana unarefuka kwenye nusutufe ya kaskazini usiku unarefuka kwenye nusutufe ya kusini.

Marejeo

  1. United States Naval Observatory (January 4, 2018). Earth's Seasons and Apsides: Equinoxes, Solstices, Perihelion, and Aphelion. Jalada kutoka ya awali juu ya 2007-10-13. Iliwekwa mnamo 2019-06-07.
  2. Astro Pixels (February 20, 2018). Solstices and Equinoxes: 2001 to 2100.
  3. KAST inatumia "sikusare", TUKI-ESD na KKK "ikwinoksi"

Viungo vya nje