Pentekoste
| Mwaka wa liturujia |
|---|
| Magharibi |
| Mashariki |
Pentekoste ni sikukuu ya dini za Uyahudi na Ukristo. Neno hili ni namba 50 kwa lugha ya Kigiriki.
Inaitwa hivyo kwa sababu ilikuwa sikukuu ya Kiyahudi iliyoadhimishwa siku ya hamsini baada ya Pasaka ya Kiyahudi. Sikukuu hii husheherekewa na Wayahudi kama "shavuot" jinsi ilivyoamriwa katika kitabu cha Mambo ya Walawi 23:16.
Kwa wafuasi wa Yesu Kristo ni ukumbusho wa umwagaji wa Roho Mtakatifu juu ya mitume na wanafunzi wengine wa Yesu na kuanzishwa kwa Kanisa siku ya 50 baada ya Pasaka au ufufuko wa Yesu.
Yaliyomo |
[hariri] Shavuot ya Kiyahudi na Pentekoste ya Kikristo
Inawezekana kusema ya kuwa baada ya kifo na ufufuko wa Yesu wanafunzi wake -ambao walikuwa wote Wayahudi- walikutana kwenye sikukuu ya Kiyahudi ya Shavuot wakati ambapo Wayahudi kutoka nchi mbalimbali walipotembelea Yerusalemu kwa hija kwenye nafasi ya sikukuu ile.
Tangu kuachana kwa kalenda ya Kikristo na kalenda ya Kiyahudi sikukuu zake kwa kawaida haziangukii siku ileile tena.
[hariri] Jina
Jina la "Pentekoste" kwa asili ni "πεντηκοστή" [ἡμέρα] (pentekostē [hēmera]) yaani (siku ya) hamsini.
[hariri] Pentekoste ya Mitume
Maelezo juu ya Pentekoste ya kwanza ya Kanisa hupatikana katika sura ya pili ya kitabu cha Matendo ya Mitume cha Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo.
Humo Mwinjili Luka anasimulia jinsi wanafunzi wa Yesu walivyokutana katika mji wa Yerusalemu siku ile ya "Pentekoste" na kupokea paji la Roho Mtakatifu. Baadaye walitoka nje wakianza mara kuhubiri juu ya Yesu Kristo mbele ya watu wengi, wakiwa wakazi wa mji huo pamoja na wageni kutoka nchi nyingi.
Kufuatana na taarifa yake siku hiyo watu takriban 3,000 walibatizwa kwa jina la Yesu na kuongezeka katika kile kikundi.
[hariri] Tarehe ya Pentekoste
Husheherekewa jumapili ya 7 baada ya Pasaka.
Katika madhehebu ya Ukristo yanayofuata kalenda ya Gregori Pentekoste itasheherekwa kwenye tarehe zifuatazo:
- 2012: 27 Mei
- 2013: 19 Mei
- 2014: 8 Juni
- 2015: 24 Mei
- 2016: 15 Mei
- 2017: 4 Juni
- 2018: 20 Mei
- 2019: 9 Juni
- 2020: 31 Mei
Makanisa ya Waorthodoksi yanayofuata kalenda ya Juliasi huwa na tarehe tofauti.