Maria kupalizwa mbinguni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Hii ni sehemu ya mfululizo kuhusu
Kanisa Katoliki
StPetersBasilicaEarlyMorning.jpg
Imani

Umoja wa Mungu
Utatu (Baba, Mwana, Roho Mtakatifu)
Umwilisho Maisha ya Yesu
Msalaba Ufufuko Kupaa
Historia ya Wokovu Ufunuo
Biblia Mapokeo Ualimu Dogma
Neema Dhambi Wokovu Sakramenti
Watakatifu Bikira Maria


Muundo

Papa: Benedikto XVI
Urika wa maaskofu Mitaguso mikuu
Kundi la Makardinali
Kanisa la Kilatini
Makanisa Katoliki ya Mashariki

Historia

Historia Ukristo
Ukatoliki Mlolongo wa Kitume
Sifa nne za Kanisa Utetezi Ekumeni
Maisha ya kiroho Amri Kumi Utawa
Sala Falsafa Teolojia
Muziki Sanaa Sayansi

Ibada

Liturujia Mwaka wa Kanisa
Ekaristi Liturujia ya Vipindi

Mapokeo ya liturujia

Liturujia ya Kilatini (Roma Milano Toledo Braga Lyon)
Liturujia ya Armenia Liturujia ya Misri
Liturujia ya Ugiriki Liturujia ya Antiokia
Liturujia ya Mesopotamia

Mchoro wa Tiziano, katika Basilika la Santa Maria Gloriosa dei Frari, Venezia.

Maria kupalizwa mbinguni ni sikukuu ya Kanisa Katoliki inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 15 Agosti. Inatokana na dogma iliyotangazwa na Papa Pius XII kwa hati Munificentissimus Deus ya tarehe 1 Novemba 1950 baada ya kusikiliza maoni ya maaskofu wote.

Fundisho hilo la imani ni kwamba Bikira Maria, mama wa Yesu, alipomaliza maisha yake duniani alichukuliwa mwili na roho mbinguni, ashiriki mapema utukufu wa Mwanae mfufuka kama alivyoshirikiana naye toka mwanzo hata mwisho wa maisha yake.

Fundisho hilo linalingana na lile la Waorthodoksi, ingawa hao hawajalitangaza kuwa dogma. Tarehe hiyo wao wanaadhimisha ya Kulala kwa Bikira Maria.

Umoja wa msimamo huo upande wa mashariki na wa magharibi wa Kanisa unatokana na mapokeo ya karne za kwanza za Ukristo, yanayoshuhudiwa na mababu wa Kanisa kama vile Efrem wa Syria, Timoteo wa Yerusalemu, Epifanio wa Salamina, Yohane wa Damasko.

[hariri] Viungo vya nje

Vifaa binafsi
Maeneo ya wiki

Vibadala
Vitendo
Urambazaji
Vifaa
Lugha zingine