Basilika

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Basilika kwa asili lilikuwa jengo rasmi lililotumika Roma kama mahali pa mikutano ya hadhara na maamuzi ya kimahakama.

Jina ni la Kigiriki (aulè basilikè, yaani ukumbi wa kifalme), hivyo linaelekeza kuona asili ya majengo hayo upande wa mashariki wa Bahari ya Kati

Kuanzia mwaka 313, Dola la Roma liliporuhusu raia kufuata Ukristo, basilika ziligeuzwa kuwa mahali pa ibada ya dini hiyo, kuanzia Kanisa kuu la Roma, maarufu kwa jina la Mt. Yohane huko Laterani.

Baadaye zikajengwa Basilika la Mt. Petro huko Vatikani, Basilika la Bikira Maria Mkuu na Basilika la Mt. Paulo nje ya kuta za jiji.

Baadaye, cheo cha Basilika kilitolewa kwa makanisa mengi mengi kutokana na umuhimu wake upande wa historia, dini na sanaa.

Hata hivyo, kuna basilika kuu na basilika dogo.