Breviari

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Breviari ya karne ya 15, (Walters Art Museum).

Breviari (kutoka Kilatini brevis, 'fupi') ni kitabu cha kiliturujia cha Kanisa la Kilatini kinachokusanya pamoja Zaburi, masomo, sala, tenzi, nyimbo nyingine na taratibu za kila siku kwa ajili ya Sala ya Kanisa inayowapasa kwanza maaskofu, mapadri, mashemasi na watawa.

Pengine jina hilo linatumika pia kwa vitabu vya namna hiyo vya Anglikana na Walutheri.

Kitabu cha sala hiyo rasmi kiliitwa Breviarium Romanum (Breviari ya Kiroma) hadi mwaka 1974, Papa Paulo VI alipotoa kitabu kipya kilichopewa jina la maana zaidi "Liturujia ya Vipindi. Hata hivyo jina la zamani linaendelea kutumika kwa kawaida katika lugha mbalimbali.

Asili ya jina ni kwamba katika karne XI kitabu hicho kilifupisha matini ya awali ili yaingie katika kitabu kimoja tu badala ya vingi (Biblia, Antiphonarium, Passionarius, Legendarius, Homiliarius, Sermologus, maandishi ya Mababu wa Kanisa, mbali ya Psalterium na Collectarium).

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Breviari za Karne za Kati[hariri | hariri chanzo]

Breviari kadiri ya ofisi za Papa kabla ya Mtaguso wa pili wa Vatikano[hariri | hariri chanzo]

Breviari nyingine za zamani[hariri | hariri chanzo]

Breviari za baada ya Mtaguso wa pili wa Vatikano[hariri | hariri chanzo]

Breviari zisizo za Kikatoliki[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Breviari kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.