Kiaramu
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kiaramu ni mojawapo kati ya lugha za Kisemiti ambazo zinapangwa kati ya lugha za Afrika-Asia pamoja na Kiebrania na nyinginezo.
Inatumika tangu miaka 3,000 iliyopita. Ndiyo lugha aliyoitumia Yesu pamoja na Wayahudi wengi wa wakati wake.
Sehemu chache za Biblia ziliandikwa kwa lugha hiyo wakati ilipokuwa imeenea zaidi kwenye Mashariki ya Kati, kabla haijashindwa na Kigiriki kwanza, na Kiarabu baadaye.
Hata hivyo watu 445,000 hivi wanaitumia hata leo.
Viungo vya nje [hariri]
- (Kiingereza) [1]
- (Kiingereza) Comprehensive Aramaic Lexicon — ya Hebrew Union College, Cincinnati
- (Kiingereza) Klabu ya Vijana wa Kanisa Katoliki la Kisiria
- (Kiingereza) Tovuti ya utafiti ya Kiisraeli
- (Kiingereza) Kuhusu matumizi ya Kiaramu huko Israeli