Ustaarabu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Ustaarabu ni aina ya utamaduni uliyoendelea. Mifano ya kwanza ilipatikana Mesopotamia watu walipoanza uzalishaji wa mahitaji yao kwa njia ya ufugaji, kilimo n.k. Taratibu walianzisha miji, serikali, sheria n.k. Vilevile walibuni uandishi uliowezesha kudumisha na kushirikisha ujuzi.