Piramidi
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(angalia jinsi watu na wanyama waonekana wadogo mbele ya majengo haya)
Piramidi (kut. Kigiriki πυραμίδα piramida) ni kati ya majengo makubwa kujengwa na binadamu tangu zamani. Kimsingi piramidi ni jengo lenye msingi wa mraba na kuta zake nne zina umbo la pembetatu zikikutana juu katikati kwenye kelele.
Ingawa jamii za kale katika maeneo mbalimbali ya dunia zilijenga piramidi, piramidi za Misri ndizo zinazofahamika na watu wengi duniani.
Piramidi za Misri zilijengwa kama makaburi ya wafalme mnamo mwaka 2000 KK. Hasa piramidi tatu kubwa za Giza karibu na Kairo zajulikana kote duniani zikihesabiwa kuwa "maajabu ya dunia" ya kale.
Piramidi za Mesopotamia au zigurat hazikujengwa kama makaburi bali kama sehemu za makaburi ikiaminiwa ya kwamba miungu wanakaa juu yao. Mara nyingi Mnara wa Babeli unaotajwa katika Biblia (Mwanzo 11) umetazamiwa kama zigurat.
Waindio wa Meksiko hasa Wamaya na Waazteki walijenga pia piramidi.
| Makala hiyo kuhusu "Piramidi" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Piramidi kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |