Piramidi za Giza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Piramidi kubwa za Giza: upande wa kushuto piramidi ya Mykerinos, katikati ya Khefren na kulia ya Kheops

Piramidi za Giza ni kati ya majengo yanayojulikana zaidi duniani. Pamoja na mava mengine ni sehemu ya makaburi ya Giza yaliyokuwa mahali pa kuzika wafalme wa Misri na wakubwa wa milki kwa muda wa miaka 2500. Ziko kando la bonde la Nile karibu na mji wa Giza takriban 15 km kutoka Kairo katika Misri.

Historia ya maeneo ya makaburi ya Giza kwa jumla[hariri | hariri chanzo]

Makaburi ya kwanza yaliajengwa hapa tangu chanzo cha milki ya Misri ya Kale takriban miaka 3,000 KK. Wakati wa nasaba ya 4 ya Misri eneo la makaburi haya liliongezeka sifa kwa sababu wafalme Kheops, Khefren na Mykerinos waliamua kujenga hapa piramidi kwa ajili ya makaburi yao wenyewe.

Kutokana na ujenzi wa makaburi ya kifalme ndugu za familia zao na maafisa wa juu walizikwa hapa pia hadi mwisho wa nasaba ya 7 ya Misri. Baada ya hapo na kwa sababu ya kuhamishwa kwa mji mkuu wa milki kwenye kusini ya nchi umuhimu wa eneo la makaburi ya Giza ulipungua. Mazishi ya maana yalitokea tena wakati wa nasaba za mwisho za Misri, katika ya vipindi vya kuvamiwa na Uajemi.

Piramidi kubwa na Sfinksi[hariri | hariri chanzo]

Eneo la makaburi ya Giza hujulikana hasa kutokana na piramidi kubwa zilizokuwa maarufu tayari katika nyakati za kale. Mwanahistoria wa Ugiriki ya Kale aliyeitwa Herodoti)) alizihesabu kati ya Maajabu Saba ya Dunia na tangu siku zile miaka 2,500 iliyopita zilitembelewa na watalii.

Piramidi tatu kubwa zinajulikana kufuatana na majina ya Kigiriki ya mafarao au wafalme wa Misri waliozikwa ndani yao: piramidi za Kheops, Khefren na Mykerinos. Piramidi za Kheops na Khefren ziko karibu kimo moja, ile ya Kheops iko kubwa kidogo lakini ile ya Khefren inaonekana kubwa kwa macho kwa sababu imejengwa juu ya ardhi ya juu kiasi kwa hiyo kwa macho ya mtazamaji inafika juu zaidi.

Jina la Kigiriki Jina la Kimisri Alitawala mnamo Kimo asilia Kimo cha leo Kipimo cha
upande wa msingi
Piramidi ya Kheops Khufru ~ 2620
- 2580 KK
146.1 m 138.75 m 230 m
Piramidi ya Khefren Khafre ~ 2558
-2532 KK
143.6 m 136.4 m 215.25
Piramidi ya Mykerinos Menkaure 2558
-2532 KK
65.55 m 62 m 102.2 m
x 104.4 m

Piramidi hizo zote hazikukaa peke zao bali zilijengwa pamoja na majengo ya kando.

  • Kila piramidi ilikuwa na hekalu mbili ambako makuhani walitoa sadaka kwa ajili ya roho za mafarao marehemu peponi. Hekalu 1 ilijengwa mbali kidogo kwenye chanzo cha barabara ya maandamano yaliyoendelea hadi hekalu ya pili karibu na piramidi. Njia hizi za maandamano yalitumiwa hasa wakati wa sherehe za kukumbuka farao.
  • Kwa kawaida malkia za farao walizikwa katika piramidi ndogo au makaburi mengine kando la piramidi kubwa. Piramidi za Kheops na Mykerinus huwa na piramidi 3 za malkia za kila mfalme. Kwenye piramidi za Khefren hakuna makaburi ya malkia yaliyotambuliwa.

Historia ya baadaye[hariri | hariri chanzo]

Tangu siku za kale watu walichukua mawe kutoka majengo ya Misri kwa kuyatumia katika majengo ya nyakati zao. Hii ni sababi ya kwamba kimo cha piramidi kimepunga na hasa mawe mazuri yaliyofunika nyuso za piramidi yamepotea.

Katika karne ya 12 BK mtawala wa Misri al-Malek al-Aziz Othman ben Yusuf alijaribu kubomoa piramidi akizitazama kama ushahidi wa upagani wa kale. Wafanyakazi walianza kukata mawe kutoka piramidi ndogo ya Mykerinos lakini ikaonekana ya kwamba kazi ya kubomoa labda ingekuwa ghali sawa na kujenga. Baada ya miezi kadhaa shughuli zilisimamishwa na hadi leo kuna pengo katika ukuta wa kazkazini.

Marejeo ya Nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Hourglass.svg Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Piramidi za Giza kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]