Nile

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Nchi za beseni ya mto wa Nile pamoja na tawimito
Nchi za beseni ya mto wa Nile pamoja na tawimito
Mto wa Nile
Jina: an-Nil (Kiarabu)
Mahali: Africa ya kaskazini-mashariki
Urefu: 6650 km
Chanzo: Luvironza />mto wa chanzo Burundi
Kimo cha chanzo: 2.700 juu ya UB
Mdomo: Mediteranea kaskazini ya Kairo/Misri
Kimo cha mdomo: 0.00 m juu ya UB
Tofauti ya kimo: 2.700 m
Tawimito ya kulia: Sobat, Nile ya buluu (Abbai), Atbara
Tawimto wa kushoto: Bahr al-Ghazal
Miji mikubwa mtoni (pamoja na vyanzo vyake): Alexandria, Assuan, Atbara, Bahri, Fajum, Giza, Jinja, Juba, Kairo, Kampala, Khartum, Kigali, Kusti, Luxor, Malakal, Omdurman, Port Said, Rabak, Tanta
Je inafaa kama njia ya maji? ndani ya Misri


Picha ya Nile kutoka chombo cha angani - (Shukrani kwa NASA)

Mto wa Nile (pia: Naili; Kiarabuالنيل‎ an-nīl) ni mto mkubwa kwa upande wa Mashariki ya bara ka Afrika. Mara nyingi hutajwa kuwa pia mto mrefu kabisa duniani kushinda mto Amazonas. Kutoka Ziwa la Viktoria Nyanza hadi mdomo wake kwenye Bahari ya Mediteranea Nile inavuka nchi za Uganda, Sudan na Misri kwa urefu wa 6,650 km.

Beseni ya Nile hukusanya maji ya eneo linalojumlisha 10% za eneo la Afrika yote au 3,349,000 km². Takriban watu milioni 250 hukalia beseni hiyo.

Jina[hariri | hariri chanzo]

"Nile" au "Naili" ni umbo la Kiingereza la jina la mto kutokana na jina lililotumiwa na Wagiriki wa Kale "Neilos" (Νεῖλος). Haijulikani Wagrikiki walipata jina hili kwa njia gani lakini lilikuwa kawaida nje ya Misri. Wamisri wa Kale waliita mto huu kwa jina Ḥ'pī au iteru linalomaanisha "mto mkubwa". Wakopti walikuwa na jina la piaro lakini tangu utawala wa Kiroma jina la Kigiriki ilizidi kutumika na Waarabu waliendelea na jina la Kigiriki pia hivyo leo hii wananchi wanasema "an-nil".

Chanzo cha Nile[hariri | hariri chanzo]

Nile ina vyanzo viwili ndivyo Nile yenyewe (inaitwa pia Nile nyeupe) inayotoka katika Ziwa Viktoria Nyanza na Nile ya buluu inayotoka katika Ziwa Tana. Majina haya ya "nyeupe" na "buluu" yana asili yao katika mji wa Khartoum ambako mito yote miwili inaunganika ilhali kila moja una rangi tofauti kutokana na udongo tofauti uliotia rangi yake kwenye maji yao.

Chemichemi za Nile ni mito yote inayopeleka maji kwenda Ziwa Viktoria Nyanza katika nchi za Tanzania, Burundi, Rwanda, Kongo, Uganda na Kenya. Chanzo inayoanza mbali kabisa ni Mto wa Luvironza huko Burundi unaoingia katika Mto wa Kagera na kufika Ziwa Viktoria Nyanza.

Mkono mwingine wa Nile inaanza Ethiopia ikiitwa Abbai au Nile ya Buluu inatoka katika Ziwa Tana.

Hakuna mapatano kabisa Nile inaanza wapi. Kawaida ya waandisha Waingereza ni kuhesabu kuanzia Ziwa Viktoria; waandishi wa mataifa mengine huwa wanaweza kuita tayari mto wa Kagera kwa jina "Nile ya Kagera".

Majina ya Nile[hariri | hariri chanzo]

Majina ya sehemu ya mto kuanzia Ziwa Viktoria hadi Khartoum ni kama yafuatayo:

  • kwa sababu ya rangi wakati wa mvua yake kutokana na udongo katika maji jina linakuwa Bahr al-Abyad kuanzia Bahr al-Ghazal hadi Khartoum
  • kuanzia Khartoum jina ni pekee Bahr an-Nil (mto wa Nile) hadi mdomo wake wa delta kwenye Mediteranea.

Matumizi wa maji ya Nile[hariri | hariri chanzo]

Tangu milenia maji ya Nile yamekuwa msingi wa maisha nchini Misri na pia kwa sehemu kubwa ya nchi ya Sudani. Katika miaka ya 1920 Uingereza kama mtawala mkoloni wa Sudan na Misri walikuwa na majadiliano juu ya ugawaji wa maji ya mto na kufikia mapatano juu ya matumizi ya maji ya mto Nile ya 1929.

Hadi leo Misri inadai ya kwamba mapatanao yale yanakataa ujenzi wa malambo na kuanzishwa kwa miradi ya umwagiliaji inayotumia maji ya Nile bila kibali cha serikali yake. Hapa Misri inadai ya kwamba nchi zote zilizokuwa koloni za Uingereza wakati ule zinafungwa na mapatano ya 1929 na hizi ni pamoja na Sudan, Uganda, Kenya, Tanzania halafu pia Ethiopia iliyopatana na Uingereza wakati ule. Nchi nyingine hazikubali na majadiliano juu ya mapatano mapya ya ushirikiano katika beseni ya Nile yanaendelea.

Africa satellite plane.jpg Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Nile kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.