Herodoti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Herodoti wa Halikarnassos.

Herodoti wa Halikarnassos (kwa Kigiriki Ἡρόδοτος Ἁλικαρνᾱσσεύς, hēródotos halikarnāsséus; 484 KK - 425 KK) alikuwa mwandishi wa historia wakati wa Ugiriki ya Kale.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Alikuwa mwenyeji wa mji wa Halikarnassos katika Asia Ndogo (Uturuki ya leo) akasafiri baadaye na kutembelea nchi nyingi, kame vile Italia, Bahari Nyeusi na Misri. Alikusanya habari nyingi kutoka kwa watu wengine pia.

Maandishi[hariri | hariri chanzo]

Herodoti ni maarufu kwa sababu alikusanya habari nyingi za historia ya kale ya mataifa ya Asia, Afrika na Ulaya. Waroma wa Kale walimwona kama "Baba wa historia".

Sehemu kubwa ya maandishi yake yamepotea; yanajulikana tu kwa sababu yanatajwa katika vitabu vingine vya kale. Lakini historia yake ya vita kati ya Wagiriki na Wajemi wakati wa karne ya 5 na 6 KK imehifadhiwa.

Kwa jumla hata wataalamu wa leo hutegemea mara nyingi habari zilizokusanywa na Herodoti juu ya Babeli, Misri, Uajemi na Ugiriki ya Kale.

Vyanzo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Herodoti kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.