Ukoo wa Yesu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kioo chenye umbo la waridi katika Basilika la Mtakatifu Denis, Ufaransa, ambacho kinaonyesha vizazi vya ukoo wa Yesu kuanzia Yese.
Kuba (jengo) ya kusini katika kanisa la Chora, Istanbul, inayoonyesha vizazi vya Yesu kuanzia Adamu.
Mfululizo wa kurasa juu ya Yesu
Jesus
Yesu Kristo na Ukristo

Umwilisho  • Utoto wa Yesu  • Ubatizo
Arusi ya Kana • Utume wa Yesu • Mifano ya Yesu  • Miujiza ya Yesu
Kugeuka sura • Karamu ya mwisho • Msalaba wa Yesu  • Maneno saba
Kifo cha Yesu  • Ufufuko wa Yesu
Kupaa mbinguni  • Ujio wa pili
Injili  • Majina ya Yesu katika Agano Jipya  • Yesu kadiri ya historia  • Tarehe za maisha ya Yesu • Kristolojia

Mazingira ya Yesu

Wayahudi • Kiaramu • Bikira Maria • Yosefu (mume wa Maria) • Familia takatifu • Ukoo wa Yesu • Ndugu wa Yesu • Yohane Mbatizaji

Mitazamo juu ya Yesu

Mitazamo katika Agano Jipya · Mitazamo ya Kikristo • Mitazamo ya Kiyahudi • Mitazamo ya Kiislamu • Yesu katika sanaa

Ukoo wa Yesu unapatikana katika vitabu viwili vya Agano Jipya: Injili ya Mathayo ambayo inaorodhesha vizazi kuanzia Abrahamu hadi kwa Yosefu (mume wa Maria), na Injili ya Luka inayorudi nyuma kuanzia Yosefu hadi kwa Adamu, aliyeumbwa na Mungu mwenyewe.

Injili hizo zote mbili zinasisitiza kwamba Yosefu si mzazi wa Yesu, kwa kuwa Bikira Maria alipata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.

Pia zinasisitiza kwamba Yesu ni Mwana wa Daudi, yaani kwa njia ya Yosefu, ambaye kinasaba anatokana na mfalme huyo maarufu wa Agano la Kale, ana haki ya kurithi cheo chake.

Hata hivyo majina mengi ni tofauti katika orodha hizo mbili, kiasi kwamba wataalamu wanatoa maelezo mbalimbali kuhusiana na desturi za Israeli wakati ule, kwa mfano katika kutumia orodha ya vizazi, na kutokana na malengo ya Wainjili hao[1][2], ambao wote wawili walitaka kusisitiza kihisabati kwamba Yesu amefika kwa wakati mwafaka uliopangwa na Mungu kwa makini (vizazi 14x3 kadiri ya Mathayo; 7x11 kadiri ya Luka).

Akiwaandikia Wayahudi, mwinjili Mathayo alitaka kusisitiza kwamba Yesu ni Daudi mpya, lakini pia mrithi wa Abrahamu katika kuwa baraka kwa mataifa yote.

Akiwaandikia watu wa mataifa, mwinjili Luka alitaka kuonyesha kwamba Yesu ni mwana wa Adamu, hivyo anahusiana na binadamu wote.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Marcus J. Borg, John Dominic Crossan, The First Christmas (HarperCollins, 2009) page 95.
  2. R. T. France, The Gospel According to Matthew: An Introduction and Commentary (Eerdmans, 1985) page 71.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ukoo wa Yesu kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.