Austria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
'Republik Österreich
Jamhuri ya Austria
Bendera ya Austria Nembo ya Austria
Bendera Nembo
Wito la taifa: --
Wimbo wa taifa: “'Land der Berge, Land am Strome
(Kijerumani kwa "Nchi ya milima, nchi ya mtoni")
Lokeshen ya Austria
Mji mkuu Vienna
48°12′ N 16°21′ E
Mji mkubwa nchini Vienna
Lugha rasmi Kijerumani 1
Serikali Jamhuri
Heinz Fischer
Werner Faymann
Uhuru
Mkataba kuhusu Austria ulianza
Tangazo la baki

27 Julai 1955
26 Oktoba 1955
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
83,871 km² (ya 115)
1.3
Idadi ya watu
 - 2006 kadirio
 - 2001 sensa
 - Msongamano wa watu
 
8,292,322 (ya 9)
8,032,926
99/km² (ya 99)
Fedha Euro () 2 (EUR)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
CET (UTC+1)
CEST (UTC+2)
Intaneti TLD .at 3
Kodi ya simu +43
1 Kislovenia, Kikroatia, Kihungaria ni lugha rasmi kieneo.
2 Kabla ya 1999: Shilingi ya Austria.Ramani ya Austria

Austria (Kijer.: Österreich) ni nchi ya Ulaya ya Kati. Imepakana na Ujerumani, Uceki, Slovakia, Hungaria, Slovenia, Italia, Uswisi na Liechtenstein. Mji mkuu ni Vienna.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Austria:Uso wa nchi
Mlima Grossglockner

Eneo la nchi lina umbo ndefu na nyembamba kama kanda linaloelekea kutoka mashariki kwenda magharibi. Sehemu kubwa ya Austria (60%) ni milima. Tambarare ziko hasa kando la mto Danubi ambao ni pia mto mkubwa. Theluthi moja la eneo liko chini ya 500 m. Zaidi ya 40% za nchi ni misitu. Mto Danubi unavuka sehemu kubwa ya nchi.

Milima mikubwa ya Austria inafikia kimo kati ya 3000 na 4000 m. Katika hali ya hewa ya nchi kuna theluji mwaka wote. Mlima mkubwa ni Grossglockner mwenye 3,798 m halafu Wildspitze mwenye 3,774 m juu ya UB.

Ziwa kubwa ni ziwa la Neusiedler See lililopo mpakani na Hungaria. Mlimani kuna maziwa mengi madogo. Uso huo wa nchi ni msingi wa utalii ulio muhimu sana Austria. Wakati wa joto watalii wanaponda baridi ya milima; wakati wa baridi wanakuja kwa kucheza ski.

Wakazi[hariri | hariri chanzo]

Watu wa Austria huzungumza Kijerumani ambacho ni pia lugha rasmi. Mpakani upande wa kusini na mashariki kuna pia wasemaji wa Kikroatia, Kislovenia na Kihungaria. Lugha hizi zina cheo rasmi kieneo au kitarafa.

Kwa jumla lahaja na utamaduni hufanana katika mengi na ile ya Wabavaria katika jimbo la jirani la Ujerumani. Kama huko wananchi wengi ni Wakatoliki.

Miji[hariri | hariri chanzo]

Hali halisi kuna jiji moja kubwa tu ambayo ni mji mkuu Wien (Vienna). Ilikua kama mji mkuu wa Kaisari wa Dola Takatifu la Kiroma na baadaye wa milki ya Austria iliyojumlisha sehemu kubwa za Ulaya ya Kusini-Mashariki.

Miji mingine mikubwa kiasi ni

Historia[hariri | hariri chanzo]

Austria kama nchi ndogo jinsi ilivyo imepatikana tangu 1918 mwishowe tangu 1945. Kwa muda mrefu wa historia yake Austria ilihesabiwa kama sehemu ya Ujerumani. Kwa karne nyingi watawala wake walishika cheo cha Kaisari wa Dola takatifu la Roma lililojumlisha Ujerumani wote. Austria ilitawala pia sehemu kubwa za Ulaya ya Mashariki.

Wakati wa vita za Napoleoni Kaisari Franz II alilazimishwa kujiuzulu kama Kaisari la Ujerumani wote mwaka 1806 akabaki na cheo cha Kaisari wa Austria tu. Baada ya Napoleoni Austria ilikuwa nchimuhimu katika shirikisho la Ujerumani. Mwaka 1866 Austria ilishindwa katika vita dhidi Prussia ikatoka katika siasa ya Ujerumani.

Hadi Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia Austria iliendelea kutawala nchi za Ulaya ya Mashariki pamoja na Uceki, Slovakia, Slovenia, Kroatia, Bosnia-Herzegovina, Hungaria na sehemu kubwa ya Poland ya Kusini, pia sehemu zilizopo sasa chini ya Italia. Mwisho wa vita dola hili liliachana na nchi ndogo iliyokaliwa na Waaustria Wajerumani ilibaki. Washindi wa vita vilizuia Waaustria wasijiunge na Ujerumani hivyo Jamhuri ya Austria ilianzishwa.

Mwaka 1938 dikteta wa Ujerumani Adolf Hitler (aliyekuwa Mwaustria mwenyewe) alivamia Austria kwa jeshi lake na kuiunganisha na Ujerumani. Wakati ule sehemu kubwa ya Waaustria walikubali.

Baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia Austria ilirudishwa kama nchi ya pekee ikabaki hivyo.

1995 Austria ikajiunga na Umoja wa Ulaya.

Majimbo[hariri | hariri chanzo]

Makala kuu: Majimbo ya Austria
Nafasi Jimbo Makao
makuu
Jina rasmi Wakazi Eneo (km²)
1 Vienna Vienna Wien 1,677,867 415
2 Austria Chini Sankt Pölten Niederösterreich 1,597,240 19,178
3 Austria Juu Linz Oberösterreich 1,408,165 11,982
4 Steiermark Graz Steiermark 1,205,609 16,392
5 Tirol Innsbruck Tirol 703,512 12,648
6 Karinthia Klagenfurt Kärnten 561,094 9,536
7 Salzburg Salzburg Salzburg 530,576 7,154
8 Vorarlberg Bregenz Vorarlberg 366,377 2,601
9 Burgenland Eisenstadt Burgenland 281,190 3,965

Waaustria Mashuhuri duniani[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Europa Mapa.png Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Austria kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.