Arnold Schwarzenegger

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Arnold Schwarzenegger (2015).

Arnold Schwarzenegger (amezaliwa tar. 30 Julai 1947 nchini Austria) ni mwigizaji wa filamu na mwanasiasa aliyekuwa gavana wa jimbo la California nchini Marekani tangu 2003 hadi Januari 2011. Arnold anaishi mjini Los Angeles, California.

Schwarzenegger alielekea nchi Marekani mnamo mwaka wa 1968 na kisha baadaye akawa mwigizaji wa filamu. Ameigiza filamu nyingi tu, ikiwemo ile ya The Terminator na nyingine nyingi tu. Mnamo mwaka wa 2003, pale Bw. Gray Davis alipoondoka madarakani, Schwarzenegger akashinda kiti cha kuwa Gavana wa California akarudishwa mwaka 2007.

Schwarzenegger ameoana na Bi. Maria Shriver.

Kabla ya kuwa mwigizaji, kwanza alikuwa Mnyanyua Vyuma. Kwa kigezo hicho akafanikiwa kushinda mashindano ya Mr. Universum kwa takriban mara saba.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons