1945
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Lango la Historia | Lango la Biografia | Karibuni | Orodha ya Miaka
◄ | Karne ya 19 | Karne ya 20 | Karne ya 21
◄ | Miaka ya 1910 | Miaka ya 1920 | Miaka ya 1930 | Miaka ya 1940 | Miaka ya 1950 | Miaka ya 1960 | Miaka ya 1970 | ►
◄◄ | ◄ | 1941 | 1942 | 1943 | 1944 | 1945 | 1946 | 1947 | 1948 | 1949 | ► | ►►
1945 ilikuwa mwaka wa mwisho wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Majaribio ya Ujerumani na Japani ya kutawala dunia yalishindwa na mataifa yalitafuta ushirikiano mpya. Ilikuwa pia chanzo cha vita baridi kati ya vikundi wa washindi wa vita kuu baada ya Umoja wa Kisovyeti kujenga utawala wake juu ya nchi za Ulaya ya Mashariki.
Matukio[hariri]
- 8/9 Mei - Ujerumani inajisalimisha; mwisho wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia katika Ulaya.
- 26 Juni - Umoja wa Mataifa unaanzishwa mjini San Francisco na kuchukua nafasi ya Shirikisho la Mataifa.
- 16 Julai - Mlipuko wa kinyuklia wa kwanza karibu na Los Alamos (Marekani): Bomu la jaribio liitwalo „Trinity“ (Utatu) lenye nguvu ya kilotani 20 za TNT.
- 6 Agosti - Bomu la atomu la kwanza linatupwa na jeshi la anga la Marekani kwenye mji wa Hiroshima (Japani). Watu 70.000 wanakufa mara moja, jumla ya wafu kutokana na majeruhi na mnururisho itafikia idadi ya watu 240.000.
- 15 Agosti - Japani inajisalimisha; mwisho wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia katika Asia.
- 17 Agosti - Nchi ya Indonesia inatanganza uhuru wake kutoka Uholanzi.
- 27 Desemba - Kuundwa kwa IMF (Shirika la Kimataifa la Fedha).
Waliozaliwa[hariri]
| Kalenda ya Gregori | 1945 MCMXLV |
| Kalenda ya Kiyahudi | 5705 – 5706 |
| Kalenda ya Ethiopia | 1937 – 1938 |
| Kalenda ya Kiarmenia | 1394 ԹՎ ՌՅՂԴ |
| Kalenda ya Kiislamu | 1364 – 1365 |
| Kalenda ya Kiajemi | 1323 – 1324 |
| Kalenda ya Kihindu | |
| - Vikram Samvat | 2000 – 2001 |
| - Shaka Samvat | 1867 – 1868 |
| - Kali Yuga | 5046 – 5047 |
| Kalenda ya Kichina | 4641 – 4642 甲申 – 乙酉 |
- 4 Januari - Richard Schrock, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia mwaka wa 2005
- 7 Januari - Raila Odinga, mwanasiasa wa Kenya
- 6 Februari - Bob Marley, mwanamuziki kutoka Jamaika
- 6 Mei - Peter Mahamudu Msolla, mwanasiasa wa Tanzania
- 8 Mei - Keith Jarrett, mwanamuziki kutoka Marekani
- 19 Juni - Aung San Suu Kyi, mwanasiasa wa Myanmar na mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Amani mwaka wa 1991
- 21 Juni - Aloysius Balina, askofu wa Jimbo Katoliki la Shinyanga, Tanzania
- 1 Agosti - Doug Osheroff, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia mwaka wa 1996
- 8 Agosti - Bruno Pius Ngonyani, askofu Mkatoliki nchini Tanzania
- 17 Agosti - Norbert Wendelin Mtega, askofu Mkatoliki nchini Tanzania
- 30 Novemba - Telesphore Mkude, askofu Mkatoliki nchini Tanzania
bila tarehe
- Thomas Mapfumo, mwanamuziki kutoka Zimbabwe
- Augustine Mrema, mwanasiasa kutoka Tanzania
- Gertrude Mongella, mwanasiasa wa kike kutoka Tanzania
Waliofariki[hariri]
- 31 Machi - Hans Fischer (mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia mwaka wa 1930)
- 9 Aprili - Dietrich Bonhoeffer, mwanateolojia nchini Ujerumani, aliuawa na Chama cha Nazi
- 12 Aprili - Franklin D. Roosevelt, Rais wa Marekani (1933-45)
- 28 Aprili - Benito Mussolini (kiongozi wa Italia) anauawa na wanamgambo Waitalia wakomunisti.
- 30 Aprili - Adolf Hitler (kiongozi wa Ujerumani) anajiua mjini Berlin pamoja na mke wake Eva.
- 26 Septemba - Bela Bartok (mtungaji wa muziki Mhungaria)
- 20 Novemba - Francis William Aston (mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia, mwaka wa 1922)
- 4 Desemba - Thomas Hunt Morgan (mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba, mwaka wa 1933)
Wikimedia Commons ina media kuhusu: