Jamaika

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Commonwealth of Jamaica
Bendera ya Jamaika Nembo ya Jamaika
Bendera Nembo
Wito la taifa: Out of many, one people (kutoka wengi - taifa moja)
Wimbo wa taifa: Jamaica, Land We Love
Wimbo wa kifalme: God Save the Queen
Lokeshen ya Jamaika
Mji mkuu Kingston
17°59′ N 76°48′ W
Mji mkubwa nchini Kingston
Lugha rasmi Kiingereza
Serikali Ufalme wa kikatiba
Elisabeth II
Kenneth Hall
Portia Simpson-Miller
Uhuru
kutoka Uingereza
6 Agosti 1962
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
10,991 km² (ya 166)
1.5
Idadi ya watu
 - Julai 2005 kadirio
 - Msongamano wa watu
 
2,651,000 (ya 138)
252/km² (ya 49)
Fedha Dollar ya Jamaika (JMD)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC-5)
(UTC)
Intaneti TLD .jm
Kodi ya simu +1-876]]

-Jamaika ni nchi ya kisiwani katika Bahari ya Karibi . Iko 150 km kusini ya Kuba na 150 km upande wa magharibi wa Haiti na kisiwa kikubwa cha tatu kati ya Antili Kubwa. Katika lugha ya Kiingereza visiwa hivi huitwa "West Indies" (visiwa vya Uhindi wa Magharibi).

Jina limetokana na neno la Arawak la "Xaymaca" au "Chaymaka" linalomaanisha "nchi ya chemchem" (yaani kisiwa chenye maji matamu).

Mji mkuu ni Kingston.

Ramani ya Jamaika

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Kisiwa kina urefu wa 240 km na upana hadi 85 km. Eneo lake ni 10.991 km². Visiwa vidogo vya Pedro Cays vyenye eneo la 23 ha jumla ni sehemu ya nchi ya Jamaika.

Mashariki ya kisiwa kuna nyororo ya milima ya buluu yenye urefu wa 100 km penye kilele cha Blue Mountain Peak (2256 m juu ya UB). Katikati kuna nyanda za juu zilizojengwa kwa mawe ya chokaa yenye mabonde marefu. Upande wa kusini nyanda za juu zina mtelemko mkali hadi mwambao wa bahari.

Iko mito mingi mifupi; mto mrefu ni Black River yenye 53.4 km. Mto wa Hector's River uns mwendo wa 6 km chini ya ardhi.

Mtelemko mkali kwenye pwani la Jamaika

Hali ya Hewa[hariri | hariri chanzo]

Haliy a hewa ni ya kitropiki. Hakuna tofauti kubwa ya halijoti mwaka wote. Halijoto ya wastani katika Kingston ni 25 °C wakati wa Januari na 27 °C wakati wa Julai.

Usimbishaji hutofautiana katika kanda mbalimbali ya kisiwa. Milima ya kaskazini-mashariki hupokea zaidi ya 5.000 mm lakini Kingston ina 813 mm pekee. Mvua inanyesha hasa Mei, Juni, Oktoba na Novemba. Miezi ya Septemba na Oktoba inaona dhoruby kali za tufani mara kwa mara.

Miji[hariri | hariri chanzo]

Miji muhimu iko mwambaoni kwa sababu ya milima ya ndani.

 • Kingston ni mji mkubwa mwenye wakazi karibu lakhi sita. Ni mji mkuu na mahali pa chuo kikuu kikubwa cha Jamaika. Mji ulikuwa na matatizo makubwa ya usalama katika miaka ya nyuma.
 • Spanish Town ni mji wa pili mwenye wakazi 145.000. Ni kitovu cha eneo la kilimo cha ndizi na miwa.
 • Mji wa Montego Bay upo katika kaskazini ya kisiwa karibu na mahali ambako Kristoforo Kolumbus alifika mara ya kwanza. Bandari yake ni mhimi kwa biashara ya nje. Ni eneo la utalii.

Wakazi[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 2006 Jamaika ilikuwa na wakazi 2,758,000. Nusu yao waliishi mjini. Umri wa wastani ni miaka 23, thluji moja ni watoto hadi miaka 14.

Takriban 90 % wa wakazi ni wa asili ya kiafrika. Mababu walikuwa watumwa kutoka Afrika waliofikishwa kisiwani katika karne ya 17 na karne ya 18. Wengina ni chotara au wa asiliy a Ulaya na Uchina. Wakazi asilia walikuwa Warawak na Wataino ambao hawako tena kama vikundi vya pekee; wengi walikufa kutokana na magonjwa ya Wazungu au vita za miaka ya kwanza baada ya kufika kwa Wahispania. Wengine walichanganywa na vikundi vingine.

Pamoja na lugha rasmi Kiingereza kuna pia aina ya Kikreoli yenye asili ya Kiingereza.

Dini[hariri | hariri chanzo]

Wakazi walio wengi hufata Ukristo hasa katika makanisa kiprotestant kama vile

 • Church of God (21,2 %)
 • Wabatisti (8,8 %)
 • Waanglikana (5,5 %)
 • Wasabato (9 %)
 • Wapentekoste(7,6 %)
 • Wakatoliki (4 %)
 • Wamethodisti (2,7 %)
 • United Church of Christ (2,7 %)
 • Brethren (1,1 %)
 • Mashahidi wa Jehova (1,6 %)
 • Moravian (1,1 %).

::(namba za asilimia ni makadirio)

Dini ya pekee ya Jamaika ni Rastafari.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Wakazi wa kwanza wa Jamaika walikuwa Wataino ambao ni kabila ya Waarawak kutoka Amerika Kusini. Walikuwa wakulima na wavuvi. Wamepotea kama utamaduni wa pekee baada ya kufika kwa Wazungu kutokana na magonjwa mageni yaliyofika na Wahispania na mauaji wakati wa vita. Waliobaki waliingia katika ndoa na Wazungu au Waafrika waliofika baadaye na kuwa sehemu ya wakazi chotara kisiwani.

Kristoforo Kolumbus alifika mwaka 1494 na kuweka kisiwa chini ya utawala wa Hispania. Aliamini ya kwamba alifika Uhindini akaita visiwa hivi "Uhindi wa Magharibi" na wenyeji wakaitwa "Indios" (kihisp. Wahindi) na baadaye mara nyingi "Wahindi wekundu".

1655 Waingereza waliteka kisiwa wakaanzisha uchumi wa mashamba makubwa ya miwa. Jamaika imekuwa mahali pakuu pa kutengeneza sukari duniani. Watumwa wengi waafrika walipelekwa kisiwani kama wafanyakazi kwenye mashamba haya. Ndio mababu wa 90% wa wakazi wa leo wa Jamaika.

Kati ya 1834 na 1838 utumwa ulifutwa.

1958 Jamaika ilianza kuingia katika uhuru kama jimbo la "Shirikisho la Uhindi wa Magharibi".

Uhuru kamili ulipatikana 1962.

Utamaduni[hariri | hariri chanzo]

Muziki ni sehemu muhimu sana katika utamaduni wa Jamaika. Hasa muziki ya Reggae imejulikana kote duniani. Mwanamuziki mashuhuri hasa wa Jamaika alikuwa Bob Marley na kikundi chake cha "The Wailers".

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Caribe-geográfico.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Bahari ya Karibi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Jamaika kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.