Vikram Samvat

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mtawa wa Jain Kalakacharya na mfalme wa Saka (Kalakacharya Katha manuscript, Chhatrapati Shivaji Maharaj Vastu Sangrahalaya, Mumbai)


Vikram Samvat (pia: Bikram Samvat, Devanagari:विक्रम सम्वत्) ni kalenda rasmi nchini Nepal. Huhesabiwa kati ya kalenda za Kihindu na kufuata muundo wa mwaka jua-mwezi (lunisolar).

Jina latokana na mfalme wa Kihindi Vikramaditya Samvat aliyetawala katika Uhindi kaskazini mnamo karne ya kwanza KK. Mwaakmpya unaanza kwenye siku ya mwezi mwanadamu wa mwezi wa Chaitra inayotokea wakati wa ama Machi au Aprili. Mwezi hufuata awamu halisi za mwezi.