Myanmar

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Myanmar long form.png
Pyi-daung-zu Myan-mar Naing-ngan-daw

Shirikisho la Myanmar
Bendera ya Myanmar Nembo ya Myanmar
Bendera Nembo
Wito la taifa:
Wimbo wa taifa: Kaba Ma Kyei
Lokeshen ya Myanmar
Mji mkuu Naypyidaw1
19°45′ N 96°12′ E
Mji mkubwa nchini Yangon
Lugha rasmi Kiburma
Serikali
Mwenyekiti
Waziri Mkuu
Halmashauri ya kijeshi
Jenerali Than Shwe
Soe Win
Uhuru
Tarehe
4 Januari 1948
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
676,578 km² (ya 40)
3.06%
Idadi ya watu
 - Julai 2005 kadirio
 - 1983 sensa
 - Msongamano wa watu
 
50,519,0002 (ya 24)
33,234,000
75/km² (ya 119)
Fedha Kyat ya Myanmar (K) (mmK)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
MMT (UTC+6:30)
{{{time_zone_DST}}} (UTC{{{utc_offset_DST}}})
Intaneti TLD .mm
Kodi ya simu +95

-

1Serikali kadhaa hutambui Yangon kama mji mkuu.


Majimbo ya Myanmar

Myanmar (pia: Myama; Myamari) ni nchi ya Asia ya Kusini-Mashariki inayojulikana pia kwa jina la Burma au Bama. Imepakana na China upande wa kaskazini, Laos upande wa mashariki, Uthai kwa kusini-mashariki, Bangladesh na Uhindi. Kuna pwani la Bahari Hindi lenye urefu wa 2,000 km.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Kaskazini ya nchi ina milima mingi. Safu tatu za Rakhine Yoma, Bago Yoma na Nyanda za Juu za Shan zimeanza katika Himalaya na kuelekea kusini. Milima ya Hengduan Shan iko mpakani na China. Mlima mkubwa ni Hkakabo Razi kwenye jimbo la Kachin mwenye kimo cha 5,881 m.

Mito mitatu mikubwa ya Myanmar inavuka kati ya safu za milima ni

Mto Ayeyarwady ni mto mkubwa wa Myanmar mwenye urefu wa 2,170 km. Bonde lake ni ya rutba lina wakazi wengi.

Karibu nusu ya nchi ni misitu.

Utamaduni[hariri | hariri chanzo]

Myanmar ni nchi ya makabila mengi na lugha nyingi. Wakazi walio wengi hufuata dini ya Ubuddha. Kundi kubwa ni Waburma wenye asili katika milima ya Tibet walikotoka mababu yao miaka 1000 iliyopita.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Tangu karne ya 9 BK nchi iliona falme mbalimbali zilizotawala kutoka mji mkuu wa Pagan. Katika karne ya 19 Uingereza ulianza kujishughulisha na habari za Burma (Myanmar) baada ya kutawala maeneo jirani ya Uhindi. Kwa vita tatu kati ya 1826 na 1885 Uingereza ulieneza utawala wake. Burma ilikuwa sehemu ya Uhindi wa Kiingereza tangu 1885. 1937 Waingereza walianza kutawala Burma kama koloni ya pekee.

Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia Japon ilitwaa karibu nchi yote. Baada ya vita Burma ikapata uhuru wake 4 Januari 1948.

Serikali iliyochaguliwa kidemokrasia ilipinduliwa 1962 kwa mapinduzi ya kijeshi. Mtawala mpya alikuwa jenerali Ne Win hadi 1988 aliyetangaza siasa ya "Ujamaa wa Kiburma". Upinzani ulikandamizwa mara kadhaa vikali.

Nchi iliona harakati kwa ajili ya demokrasia na dhidi ya udikteta mwaka 1988. Ne Win alijiuzulu. Baada ya maandamano yaliyokandamizwa mara kadhaa Jenerali Saw Maung alichukua utawala kwa nguvu ya kijeshi. Uchaguzi huru wa 1989 ilileta ushindi wa chama cha NLD, chini ya Aung San Suu Kyi. lakini kamati ya kijeshi ilikataa kukabishi serikali.

Burma ilibadilishwa jina kuitwa "Myanmar" ikaendelea kutawaliwa na serikali ya kijeshi. Upinzani hauruhusiwi.

Picha[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iran | Iraq | Israel | Japan | Kambodia | Kazakhstan | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Kirgizstan | Laos | Lebanon | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Urusi1 | Saudia | Singapore | Sri Lanka | Syria | Taiwan (Jamhuri ya China) | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Ufilipino | Uthai | Uturuki1 | Turkmenistan | Uhindi | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi hii iko Asia lakini kwa sababu za kihistoria au kiutamaduni inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya. 3. Eneo la pekee la China.


BlankAsia.png Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Myanmar kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.