Tibet

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
            Tibet ya kihistoria jinsi inavyodaiwa na harakati za uhuru kwa nchi
Maeneo ya Watibet jinsi yanavyotajwa na Jamhuri ya Watu wa China
Eneo la Mkoa wa kujitawala wa Tibet ndani ya China (hali halisi)
Eneo linalodaiwa na Uhindi
Eneo linalidaiwa na China kama sehemu ya Mkoa wa kujitawala wa Tibet
Maeneo mengine ambayo kihistoria yalikuwa chini ya athira ya Tibet
Ramani ya Tibet ya Kichina.

Tibet ni nchi katika milima ya Himalaya ya Asia.

Mji mkuu ni Lhasa.

Upande wa dini, Watibet walio wengi ni Wabuddha.

Tibet imekuwa sehemu ya Jamhuri ya Watu wa China tangu miaka ya 1950.

Ni kwamba mwaka 1951 China ilishambulia jeshi la Tibet ikalazimisha serikali ya Tibet kukubali ya kwamba ni sehemu ya China kwa ahadi ya kwamba mambo ya ndani yataendelea jinsi yalivyokuwa awali.

Lakini mnamo 1958 maafisa wa China walianza kumtendea Dalai Lama (kiongozi wa Tibet) kwa dharau. Dalai Lama alikimbilia Uhindi na jeshi la China likakandamiza harakati ya watu ya kurudisha uhuru wa nchi.

Tangu mwaka 1959 kuna Watibet wengi wanaokaa Nepal na Uhindi kama wakimbizi. Ndani ya Tibet idadi ya walowezi Wachina iliongezeka.