Ramani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Ramani ya dunia ya 1662
Ramani yaonyesha kilele cha mlima Kilimanjaro na mistari ya kimo
Ramani ya muundo wa usafiri wa reli ndani ya mji wa London


Ramani ni picha -kwa awaida mchoro- ya dunia au sehemu au sifa zake. Ni tofauti na picha iliyopigwa kwa kamera kutoka ndege au chombo cha angani kwa sababu mchora ramani anaamua anachotaka kuonyesha na kuzipa uzito sifa anazotaka kuweka mkazo.

Kuna aina nyingi za ramani.

  • ramani za topografia huonyesha uso wa dunia (kwa mfano: bahari, nchi, milima, mito, kimo cha ardhi na kina cha bahari)
  • ramani za sifa huonyesha sifa fulani kuhusiana na dunia (kwa mfano: historia, uchumi, usambazaji wa wakazi katika nchi n.k.)
  • ramani inaweza kufuata uso wa dunia
  • ramani inaweza kufuata mahitaja ya mtazamaji (ramani ya njia ya reli huonyesha mstari tu na ufuatano wa vituo bila kutaja kona na mabadiliko ya mwelekeo)

Kila mchora ramani anahitaji kuamua jinsi ya kuonyesha mambo yake. Kwa ramani za kijiografia tatizo hutokana na umbo la dunia ambayo ni tufe wakati ramani kwa kawaida ni karatasi bapa.

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

xc:Tamil

Sciences de la terre.svg Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ramani kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Kigezo:Link FA