Jenerali

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jenerali wa nyota 4 George S. Patton mnamo 1945, mwishoni mwa Vita vya Kidunia vya pili

Jenerali ni cheo kikuu cha kijeshi katika nchi nyingi za dunia. Jenerali huwa kiongozi wa ngazi ya juu katika jeshi.

Idadi ya majenerali si kubwa. Kazi yao ni kuongoza na kupanga kazi ya jeshi. Kwa kawaida hawashiriki wenyewe katika mapigano.

Neno limeingia katika Kiswahili kutoka lugha ya Kiingereza. Asili yake ni Kilatini "generalis" yenye maana ya "kwa ujumla".

Vyeo vya kijeshi - Tanzania

Jenerali * Luteni Jenerali * Meja Jenerali * Brigedia * Kanali * Luteni Kanali * Meja * Kapteni * Luteni * Luteni-usu

Afisa Mteule Daraja la Kwanza * Afisa Mteule Daraja la Pili * Sajinitaji * Sajenti * Koplo * Koplo-usu