San Francisco

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Jiji la San Francisco
Skyline ya Jiji la San Francisco
Nchi Marekani
Jimbo California
Kitongoji San Francisco
Website: www.sfgov.org
Mahali pa San Fransisco katika Kalifornia
Reli ya manisipaa aina ya Cable Car
Bendera ya San Francisco

San Francisco ni mji wa Marekani uliopo kwenye mwambao wa Pasifiki katika jimbo la Kalifornia. Ni mji mkubwa wa nne wa Kalifornia ukiwa na wakazi 744,000.

San Francisco iko kwenye rasi kati ya Pasifiki na hori la San Francisco. Mlangobahari wa kuingia katika hori huitwa "Golden Gate".

Mji ulianzishwa na Wafransisko Wahispania mnamo 1776 kama sehemu ya koloni lao la Meksiko. Jina limechaguliwa kwa heshima ya mwanzilishi wao, Mt. Fransisko wa Asizi.

Baada ya vita ya Marekani dhidi ya Meksiko ya 1846 mji ukawa sehemu ya Marekani. Uchimbaji wa dhahabu ulisababisha ukuzi wa haraka.

1906 San Francisco iliharibiwa na tetemeko la ardhi ikajengwa upya.

Mji hutembelewa na watalii wengi wanaopenda kuangalia daraja la Golden Gate, kisiwa cha Alcatraz na gereza lake, halafu kuzunguka mjini kwa reli za nyaya.

Mji unajulikana pia kwa jumuiya kubwa za mashoga na wabasha.

[hariri] Tovuti za Nje

Flag USA template.gif Makala hii kuhusu maeneo ya Marekani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu San Francisco kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.