Daraja

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Daraja juu ya mto

Daraja ni jengo lililoundwa kwa kusudi la kuwa na njia juu ya pengo au kizuizi. Mfano mzuri ni daraja linaloendeleza barabara juu ya mto, bopo au juu ya barabara nyingine.

Kuna aina nyingi za madaraja. Ukubwa wa daraja unategemea upande mmoja upana wa kizuizi kinachotakiwa kuvukiwa yaani upana wa mto au bopo na kwa upande mwingine uzito wa mizigo itakayopita daraja. Daraja la kuvukisha watu halina mzigo mkubwa lakini daraja linalopokea njia ya reli au barabara kuu litabeba uzito mkubwa.

Kuna pia madaraja yanayovusha mfereji juu ya mto hivyo kuwezesha meli kupita juu ya meli nyingine. Kwa jumla madaraja ni sehemu muhimu za miundombinu wa kila nchi.

Madaraja marefu duniani [hariri]

Daraja ndefu duniani ni Bang Na Expressway mjini Bangkok (Uthai) yenye urefu wa kilomita 54. Inapitisha barabara kuu ya mpito juu ya eneo la jiji. Daraja ndefu la pili ni Lake Pontchartrain Causeway inayovuka ziwa Pontchartrain karibu na mji wa New Orleans (Marekani) lenye urefu wa kilomita 38. Madaraja haya yanasimama juu ya nguzo zinazokaa karibu kwa sababu nafasi ya chini si vigumu.

Daraja linaloning'ania [hariri]

Daraja linaloning'ania la Akashi

Ugumu wa kujenga daraja ni kuwa zaidi kama nafasi ya kuvukia ni mkono wa bahari na maji yana kina kikubwa. Hapa haiwezekani kuwa na nguzo nyingi na hapa aina ya daraja linaloning'inia inatumiwa. Daraja kubwa linaloning'ania duniani ni daraja la Akashi-Kaikyo (Japani) lenye upana wa kilomita 2 kati ya nguzo za katikati.

Madaraja ya kwanza yalitengenezwa kwa ubao. Baadaye watu waliendelea kutumia mawe. Tangu karne ya 18 madaraja ya chuma yalianza kujengwa. Baadaye madaraja mengi yamejengwa kwa kutumia saruji pamoja na feleji.

Aina za madaraja juu ya njia ya maji [hariri]

Daraja la kukunjwa
Daraja linalopandishwa
Daraja linalogeuzwa
Daraja la mfereji kuvuka mto


Science-symbol-2.svg Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Daraja kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.