Reli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Njia ya reli
Tren a las nubes cruzando Viaducto la Polvorilla.jpg
Kituo cha reli mjini Mumbai. Reli ya Uhindi inabeba abiria milioni 17 kila mwaka [1] iko kati ya reli kubwa duniani.[2]

Reli (kutoka Kiing. rail / railroad) ni usafiri wa abiria na mizigo kwa magari yanayotembea kwenye njia ya pau za feleji. Reli huwa ni sehemu muhimu za miundombinu wa kila nchi.

Kwa nchi nyingi huu ni mtindo muhimu wa usafiri kwa sababu inarahisisha mwendo wa watu na bidhaa. Ikitumiwa vema gharama zake ni afadhali kuhusu usafiri wa barabarani. Mahitaji ya nishati kwa kiwango cha mzigo ni kidogo kuliko barabarani.[3]

Faida yake ni hasa tabia za njia yake; pau za feleji huwa na uso tambarare isiyonyoka kwa hiyo magurudumu ya treni hutembea kwa msuguano mdogo.

References[hariri | hariri chanzo]

  1. http://news.bbc.co.uk/2/hi/south_asia/6287152.stm
  2. http://www.indianembassy.org/i_digest/2004/jan_31/indian_railways.htm
  3. Railroad Fuel Efficiency Sets New Record- American Association of Railroads
ThreeCoins.svg Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Reli kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.