Gurudumu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Magurudumu ya ubao

Gurudumu ni mtambo mwenye umbo la duara. Linaruhusu gari kutembea; magurudumu yanazunguka na kitu juu yake yanaenda mbele kwa kutumia nguvu kidogo.

Gurudumu linapunguza msuguano; badala ya msunguano wa kitu chote kinachosogea mbele kwenye ardhi kuna msuguano wa sehemu ndogo ya gurudumu na msuguano wa gurudumu kwenye mhimili wake. Msuguano kati ya mhimili na gurudumu unapunguzwa kwa njia ya kutia mafuta au kuweka gololi kati ya gurudumu na mhimili.

Sehemu kubwa ya usafiri kwenye nchi kavu hutegemea magurudumu kwa mfano motokaa, lori, reli ya kawaida na baisikeli. Magurudumu ni pia sehemu kubwa ya machine nyingi.

[hariri] Historia

Wataalamu wa historia huamini ya kwamba watu wa Babeli walikuwa wa kwanza kugundua gurudumu na kulitumia tangu mwaka 4000 KK. Watu wa China ya Kale waliligundua pia mnamo 2800 KK.

Ustaarabu za Amerika ya Kale kama Inka na Azteki waligundua gurudumu pia likatumiwa kwa vitu vya kucheza watoto lakini halikuwa na matumizi ya kikazi.

WikiLettreMini.svg Makala hiyo kuhusu "Gurudumu" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri".

Ikiwepo makala kuhusu Gurudumu kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili.

le