Baisikeli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Baisikeli ya kwanza ilivyobuniwa na Drais
Baisikeli za zamani
Baisikeli ya kisasa
Njia ya pekee kwa baisikeli

Baisikeli (kutoka Kilatini "bis" mara mbili na Kigiriki "κύκλος" (kiklos) = duara kupitia Kifaransa/Kiingereza bicycle) ni chombo cha usafiri kinachoendeshwa kwa nguvu ya musuli ya kibinadamu.

Baisikeli huwa na magurudumu mawili yanayoshikwa na fremu, kiti kimoja, kanyagio, breki na usukani. Kwa kawaida nguvu hupelekwa kwa nyororo kutoka kanyagio kwenda gurudumu la nyuma. Tabia nyingine za kawaida ni taa za mbele na nyuma. Magurudumu huwa na matairi yanayojaa hewa. Baisikeli bora huwa pia na gia zinazorahisisha kazi ya kukanyaga kanyagio.

Katika nchi nyingi basikeli ni chombo muhimu cha usafiri. Zamani baisikeli ilikuwa usafiri wa maskini lakini pia katika nchi kadhaa zilizoendelea watu hutumia baisikeli ama kwa usafiri wa mjini au kwa burudani. Sayansi imegundua ya kwamba baisikeli ni usafiri wa haraka mjini katika umbali wa kilomita chache. Katika nchi nyingi kuna njia za pekee kwa ajili ya baisikeli kando la barabara ya magari.

Baisikeli ni usafiri unaotumia nichati kidogo na kuwa nafuu kwa utunzaji wa mazingira.

Mashindano ya baisikeli ni tawi muhimu ya michezo ya kimataifa.

[hariri] Tazama pia

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


ThreeCoins.svg Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Baisikeli kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Vifaa binafsi
Maeneo ya wiki

Vibadala
Vitendo
Urambazaji
Vifaa
Lugha zingine