Nguruwe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Nguruwe
Nguruwe mweusi
Nguruwe mweusi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Artiodactyla (Wanyama wanaokanyaga kwa kwato mbili-mbili))
Nusuoda: Suina (Wanyama kama nguruwe)
Familia: Suidae (Wanyama walio na mnasaba na nguruwe)
Jenasi: Babyrousa Perry, 1811

Hylochoerus Thomas, 1904
Phacochoerus Cuvier, 1826
Porcula Hodgson, 1847
Potamochoerus Gray, 1854
Sus (Linnaeus, 1758)

Nguruwe ni wanyama wa familia Suidae. Nguruwe-kaya hufugwa kote duniani. Spishi mbili zinaitwa ngiri.

Spishi za Afrika[hariri | hariri chanzo]

Spishi za Asia[hariri | hariri chanzo]

Maelezo na tabia[hariri | hariri chanzo]

Nguruwe ana pua kubwa, macho madogo na mkia mdogo unaokuwa umejikunja na mfupi, ulopinda au ulonyooka. Huwa anamwili mkubwa, miguu mifupi na nywele zilizojiviringisha. Ana kwato nne kwa kila mguu, huku mbili kubwa za mbele zikitumika kutembelea. [1]

Kuzaa huwezekana msimu wote wa mwaka katika ukanda wa tropiki, lakini hasa misimu ya mvua. Nguruwe jike huweza kubeba mimba akiwa na miezi 8 mpaka 18. Kisha ataanza kupata hedhi kwa muda wa siku 21 kama hajashika mimba. Nguruwe dume huweza kushiriki maswala ya uzazi katika umri wa miezi 8 mpaka 10. [2] Kwa uzao mmoja, wanaweza kupatikana watoto 6 mpaka 12, waitwao vibwagala. [3] Kisha kuachishwa kunyonya, familia mbili au tatu zinaweza kuishi pamoja mpaka msimu mwingine wa kujamiiana.

Nguruwe hawana tezi za jasho, [4]hivyo nguruwe hujipoza kwa kutumia maji au matope wakat wa joto kali. Pia hutumia matope kama njia ya kijikinga na kuunguzwa na jua. Zaidi, matope huzuia wasiathiriwe na inzi na vijidudu. [5]

Nguruwe wanaofugwa nyumbani hukuzwa na wakulima kwaajili ya nyama na ngozi. Nywele zao ngumu hutumika pia kwa kutengeneza brashi. Baadhi ya spishi za nguruwe, kama vile wale wa Asia, pot-bellied pig, huwekwa kama wanyama wa ndani wapenzi.

Chakula[hariri | hariri chanzo]

Nguruwe ni omnivora, yaani wanakula nyama na majani. Nguruwe hula mabaki na hujulikana kwa kula chakula chochote, kujumuisha wadudu, minyoo, magamba ya miti, takataka na hata nguruwe wengine. Wakiwa mwituni hula majani, nyasi, mizizi, matunda na maua. Kwa nadra, nguruwe wakiwa wanafugwa, huweza kula watoto wao kama wakichukuzwa sana.

Nguruwe wa kawaida wana kichwa kikubwa iliyoimarishwa kwa mfupa mgumu na mduara wa tishu ngumu mbele. [6] Pua hiyo hutumika kuchimba udongo ili kutafuta chakula na ni ogani yenye uwezo mkubwa wa kuhisi.

Nguruwe huwa na seti kubwa ya meno 44. Meno chonge, na huendelea kukua na huchongwa na misuguano ya meno yenyewe. [7]

Nguruwe wanaochungwa mwituni kwa msaada wa wachungaji, wanauwezo mkubwa wa kunusa, na hutumika kutafuta uyoga katika nchi nyingi za Ulaya.

Nguruwe wafugwao[hariri | hariri chanzo]

[[8]] Mkulima wa Swideni na kitoto cha nguruwe (kibwagala) mapema karne ya 20

Nguruwe wa nyumbani ( Sus scrofa domesticus ) ambao hutambulika kwa jina la kisayansi Sus scrofa. Walianza kufugwa karibu miaka 5,000 mpaka 7,000 iliyopita. Walizaliwa na rangi yangi ya kahawia na kuendelea kuwa wa kijivu. Meno chonge ya juu huwa kama ndovu za kipekee zilizopinda nje na kuelekea juu. Urefu wa meno yao huweza kufikia milimita 900 – 1800 na uzito wa kg 50 – 350.

Nguruwe wanaakili na huweza kufundishwa kazi na mbinu ndogondogo. Hivi karibuni, wamefurahia kupewa nafasi kama wanyama kipenzi wa ndani na, hasa wale nguruwe wadogo.

Nguruwe na tamaduni[hariri | hariri chanzo]

Nguruwe mara nyingi hutumiwa kwenye utamaduni na ni mada maarufu kwenye misemo na nukuu maarufu.Nguruwe kwenye dini[hariri | hariri chanzo]

[[9]] Mchoro wa Mt. Anthony na michoro ya nguruwe nyuma yake.

• Kwa dini ya Wahindu mungu Vishnu alichukua umbo la nguruwe dume varaha kwaajili ya kuikoa dunia na pepo aliyekuwa ameivuta mpaka kilindini mwa Bahari.

• Nguruwe ni mmoja kati ya mzunguko wa wanyama 12 ambao wanatokea kwenye kalenda ya kichina ya Chinese zodiac. Waamini wa elimu ya anga katika wanaamini kila mnyama ana maana fulani pekee.

Picha[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

1. ^ Production, Supply and Distribution Online Query, United States Department of Agriculture, Foreign Agricultural Service 2. ^ Swine Summary Selected Countries, United States Department of Agriculture, Foreign Agricultural Service, (total number is Production (Pig Crop) plus Total Beginning Stocks 3. ^ Feral Pig / Hog / Pig / Wild Boar Hunting 4. ^ a b c d ADW: Sus scrofa: Information 5. ^ a b Pigs (2006) 6. ^ Managing Heat Stress In Outdoor Pigs 7. ^ Huet, 1888 8. ^ Müller, 1838 9. ^ Heude, 1892 10. ^ Heude, 1888 11. ^ Müller & Schlegel, 1843 12. ^ Groves, 1997 13. ^ Nehring, 1886 14. ^ a b Linnaeus, 1758 15. ^ Müller, 1840 16. ^ FUNK, STEPHAN M., SUNIL KUMAR VERMA, GREGER LARSON, KASTURI PRASAD, LALJI SINGH, GOUTAM NARAYAN AND JOHN E. FA (2007). The pygmy hog is a unique genus: 19th century taxonomists got it right first time round. Molecular Phylogenetics and Evolution, Volume 45, Pages 427-436 17. ^ Rosenberg M, Nesbitt R, Redding RW, Peasnall BL (1998). Hallan Cemi, pig husbandry, and post-Pleistocene adaptations along the Taurus-Zagros Arc (Turkey). Paleorient, 24(1):25–41. 18. ^ Vigne JD, Zazzo A, Saliège JF, Poplin F, Guilaine J, Simmons A. (2009). Pre-Neolithic wild boar management and introduction to Cyprus more than 11,400 years ago. Proc Natl Acad Sci U S A. 106:16135–16138. PMID 19706455 doi:10.1073/pnas.0905015106 19. ^ Giuffra E, Kijas JM, Amarger V, Carlborg O, Jeon JT, Andersson L. (200). The origin of the domestic pig: independent domestication and subsequent introgression. Genetics. 154(4):1785-91. PMID 10747069 20. ^ Sacrifice Goats, female or male. 21. ^ Ecology of Sus scrofa, Global Invasive Species Database, The Invasive Species Specialist Group 22. ^ Pig Health 23. ^ Marie Parsons. "Pigs in Ancient Egypt" 24. ^ Pros and Cons of Potbellied Pigs 25. ^ McClung, Robert M., "The New Book of Knowledge: Pigs"

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Imerekebishwa kutoka "http://en.wikipedia.org/wiki/Pig"