Ngiri
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Phacochoerus)
| Ngiri | ||||||||||||||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Dume la ngiri wa kawaida
|
||||||||||||||||
| Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Ngiri ni wanyama wa jenasi Phacochoerus katika familia Suidae. Hawa ni aina za nguruwe-mwitu wenye sugu kubwa kichwani, madume hasa (sababu ya jina kwa Kiingereza: warthog). Wana pamba ndefu, zile za dume ndefu kuliko zile za jike. Hula manyasi, mizizi, beri na matunda mengine, gamba la miti, nyoga na hata mayai, mizoga na pengine wadudu na wanyama wadogo. Wakila hupiga magoti ya mbele na wakitoroka kitisho huweka mkia juu wima.
Spishi [hariri]
- Phacochoerus aethiopicus, Ngiri-jangwa (Desert Warthog)
- Phacochoerus a. aethiopicus, Ngiri wa Afrika Kusini (Cape Warthog) imekwisha sasa (1865)
- Phacochoerus a. delamerei, Ngiri Somali (Somali Warthog)
- Phacochoerus africanus, Ngiri wa Kawaida (Common Warthog)
- Phacochoerus a. aeliani, Ngiri wa Eritrea (Eritrean Warthog)
- Phacochoerus a. africanus, Ngiri wa Nolan (Nolan Warthog)
- Phacochoerus a. massaicus, Ngiri Mashariki (Central African Warthog)
- Phacochoerus a. sundevallii, Ngiri Kusi (Southern Warthog)
Picha [hariri]
Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.