Ngurunguru

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Ngurunguru
Dume la ngurunguru (Oreotragus oreotragus)
Dume la ngurunguru
(Oreotragus oreotragus)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyana wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Artiodactyla (Wanyama wenye vidole viwili au vinne mguuni)
Nusuoda: Ruminantia
Familia: Bovidae (Wanyama walio na mnasaba na ng'ombe)
J.E. Gray, 1821
Nusufamilia: Antilopinae (Wanyama walio na mnasaba na ng'ombe)
Jenasi: Oreotragus (Ngurunguru)
A. Smith, 1834
Spishi: O. oreotragus
Zimmermann, 1783
Usambazaji wa ngurunguru
Usambazaji wa ngurunguru

Ngurunguru au mbuzi mawe (Oreotragus oreotragus) ni swala wadogo wanaotokea Afrika kusini kwa Sahara tu. Jina “mbuzi mawe” ni kielekezi cha makaza yao: maeneo yenye mawe na majabali mengi. Swala hawa ni wadogo wenye kimo cha sm 58 begani. Wana rangi ya kahawa hadi kijivu, karibu na zaituni, na vidoa vidogo vyingi. Rangi hii inafanana na rangi ya majabali ambapo wanaishi na kwa sababu ya hii hawaonekani vizuri kutoka umbali mkubwa. Madume wana pembe za sm 10-15. Katika Afrika ya Mashariki majike wana pembe pia mara nyingi. Wanyama hawa wasimama kwa ncha za kwato zao na wanaweza kubana kwato nne zote juu ya kipande cha jabali kwa upana wa sarafu kubwa. Hula mimea inayomea kati ya majabali. Hawana haja ya kunywa, kwa sababu wapata maji ya kutosha kutoka chakula chao.

Nususpishi[hariri | hariri chanzo]

Jike la ngurunguru

Sikuhizi nususpishi O. o. porteousi inafahamika tu.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.