Sahara

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Sahara jinsi inavyoonekana kutoka angani
Oasisi katika Sahara (Libya)
Matuta ya mchanga katika Sahara
Kumwagilia mashamba katikati ya Sahara

Sahara ni jangwa kubwa kabisa Afrika na jangwa ya tatu kwa ukubwa ulimwenguni baada ya Aktiki na Bara la Antaktiki. Ina eneo la kilometa za mraba 9,065,000 sawa na eneo la Marekani au karibu sawa na eneo lote ya Ulaya. Jina lake ni neno la Kiarabu (صحراء sahra' ) linalomaananisha "jangwa".

Wataalamu wa jiografia huamini ya kwamba Sahara haikuwepo wakati wote. Kutokana na utafiti wa dalili katika udongo na mawe yake eneo la Sahara katika milenia zilizopita lilikuwa na mfululizo wa vipindi vya ukame na vipindi vya mvua.

Eneo[hariri | hariri chanzo]

Sahara iko kaskazini ya Afrika. Imepakana na nchi za Moroko, Algeria, Tunesia na Libya upande wa kaskazini. Upande wa kusini ni nchi za kanda la Sahel. Upande wa magharibi Sahara inaaza kwenye pwani la Atlantiki ikielekea hadi pwani la Bahari ya Shamu kwa 5000 km. Oasisi wa mto wa Nile inakata eneo lake.

Nchi zenye sehemu kubwa ya maeneo yao katika Sahara ni hizi: Misri, Libya, Mali, Niger, Chad, Sudan, Mauretania, Sahara ya Magharibi, Moroko, Algeria und Tunisia.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Hali ya hewa ni la joto na yabisi. Halijoti ni kati ya +58 °C wakati wa mchana ikishuka usiku hadi +13 °C (mlimani hadi -10 °C). Wastani ya mvua katika Sahara ni 45.5 mm kwa mwaka lakini kuna miaka bila mvua wowote.

Kuna milima mikubwa kama milima ya Ahaggar, Tibesti na Aïr. Mlima mrefu ni Emi Koussi (3415 m) kwenye milima ya Tibesti katika Chad.

Jiolojia[hariri | hariri chanzo]

Sahari haikuwa jangwa wakati wote. Michoro ya watu wa zamani inaonekana katika milima ya Tibesti na Air inayoonesha watu wavindaji na wanayama kama viboko na mamba wanaohitaji maji mengi. Wataalamu wamegundua kutokana na utafiti wa mawe na udongo ya kwamba eneo la Sahara ilikuwa na vipindi vikavu na vipindi vya mvua mwingi.

Mnamo miaka 7000 iliyopita Sahara ilikuwa eneo nusu yabisi penye maji katika mito mirefu. Labda inawezekana kuilinganisha na Kenya ya Kaskazini ya leo. Watu walivinda na kufuga wanyama. Mnamo miaka 5000 iliyopita Sahara ilikauka kufikia hali yabisi kama leo. Lakini maji ya mvua ya nyakati zile bado yapo chini ya ardhi. Misri na Libya ina miradi mikubwa kutumia maji yale kwa pampu na kuanza kilimo jangwani kabisa.Kigezo:Link FA