Nyasi
Manyasi ni kundi la mimea inayofunika udongo; manyasi yaliyo mengi si kubwa sana lakini aina kama mianzi hufikia urefu wa miti. Kibiolojia kujumlishwa katika familia ya Poaceae au Gramineae.
Manyasi huwa na mizizi mirefu inayoshika ganda la juu la ardhi hivyo kuzuia au kupunguza mmemenyuko wa udongo. Kiekolojia aina za manyasi zimezoea mazingira tofauti kabisa kati ya kanda za joto hadi kanda za baridi sana. Wakati wa baridi au ukame majani juu ya ardhi hukauka hata kupotea kabisa lakini mizizi ina uwezo kulala uda mrefu na kusubiri mvua au halijoto ya juu zaidi.
Yaliyomo |
[hariri] Lishe ya wanyama
Watu wametumia manyasi kwa shughuli mbalimbali. Nyasi ni muhimu kama lishe ya wanyama kama ng'ombe au kondoo. Wanyama wengi wa pori wanakula nyasi vilevile. Wakulima wanaweza kuteua aina za manyasi zinazofaa kama lishe ya mifugo na kuzipanda.
[hariri] Nafaka
Aina kadhaa za manyasi hutoa mbegu zinazoliwa na watu kama nafaka; manyasi haya ya nafaka kama vile mahindi, mpunga au ngano ni kati ya vyakula vya kimsingi vya binadamu duniani.
[hariri] Mimea kwa burudani
Katika mazingira ya mjini manyasi ya pekee hutumiwa kufunika ardhi hasa katika maeneo ya bustani za mjini yanayokanyagwa na watu wengi wanaopenda kukalia kwenye manyasi na kupumzika; aina hizi zinatumiwa pia kwenye viwanja vya michezo.
[hariri] Majina kwa aina za manyasi katika Afrika ya Mashariki
- fefe (kuezeka paa, Hyparrhenia rufa - en: thatching grass, Jaragua grass)
- gomba kanzu au majani ya Pemba (Stenotaphrum dimidiatum - en: Pemba grass)
- inde (Panicum maximum - en: Guinea grass)
- kichoma-mguu, kichoma-nguo au kishona-nguo (Heteropogon contortus - en: Black Spear Grass)
- kifungambuzi (Eleusine indica - en: Indian goosegrass, Wiregrass)
- kimbugibugi (Dactylotenium aegyptium - en: Egyptian crowfood grass)
- lugowi (Cynodon spp. - en: Bermuda grass, African starr grass)
- mabingobingo (Pennisetum purpureum - en: Napier grass, elephant grass)
- malamata (Setaria verticillata - en: Bristly foxtail, love grass)
- mbaya (Rottboellia cochinchinensis - en: Guinea-fowl grass, itch grass)
- mchaichai (Cymbopogon citratus - en: Lemon grass)
- mkekundu (Chloris gayana - en: Rhodes grass)
- mtimbi au msufi wa bara (Imperata cylindrica - en: Speargrass, swordgrass, lalang grass)
- mzumai (Chrysopogon zizanioides - en: Vetiver, Khuskhus grass)
- sangari (Digitaria abyssinica - en: Couch grass)
- tete (Phragmites australis - en: Common reed)