Mpunga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mpunga
(Oryza sativa)
Mpunga
Mpunga
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Planta (mimea)
Faila: Magnoliophyta (mimnea yenye maua)
Ngeli: Liliopsida au Monocotyledones, Monocotes (mimea yenye jani asilia moja tu katika mbegu)
Oda: Poales (aina za manyasi)
Familia: Poaceae (manyasi)
Jenasi: Oryza (L.)
Mama anatoa miche ya mpunga kabla ya kuipanda shambani
Shamba la mpunga Bangladesh
Mpunga umeiva (Marekani)
Mpunga kabla ya mavuno nchini Japani
Mavuno ya mpunga nchini Hispania

Mpunga ni mmea wa familia ya manyasi katika ngeli ya monokotiledoni. Mbegu za mpunga zikisafishwa huitwa mchele na mchele ukipikwa ni chakula cha wali. Wali ni chakula muhimu cha watu katika sehemu nyingi za dunia hasa Asia lakini pia Afrika na penginepo.

Yaliyomo

[hariri] Historia ya mpunga

[hariri] Asia

Asili ya mpunga iko katika Asia. Wataalamu huamini ilipatikana mwanzoni ama China ya kusini au Uhindini. Wengine huona ya kwamba manyasi ya aina Oryza sativa yaliendelezwa na wakulima China na Uhindi kila mahali bila kutegemeana. Wakulima waliona manyasi yenye mbegu nzito kushinda manyasi mengine waliteua yale yaliyokuwa kubwa hasa na kuyapanda kwenye matuta ya bustani. Kwa njia hiyo manyasi yenye nafaka nzito yalipatikana. Wataalamu wa akiolojia walitambua alama za mpunga na matumizi yake katika mabaki yenye asili ya mwaka 6000 KK katika China na mwaka 5000 katika Uhindi.

Mnamo karne ya 3 KK mpunga ulipelekwa Japani kutoka China na kuwa chakula kikuu.

[hariri] Afrika

Aina nyingine ya Oryza glaberrima ilikuzwa katika Afrika ya Magharibi. Baadaye Waarabu walileta aina ya Kiasia iliyopandwa zaidi kutokana na mavuno makubwa.

[hariri] Uenezaji

Kutoka Bara Hindi mpunga ulipelekwa magharibi. Waroma wa Kale walijua mpunga wakala wali iliyolimwa Misri. Baadaye Waarabu walipeleka mpunga wa aina ya O. sativa katika sehemu mbalimbali za Afrika.

Wahispania na Wareno walipeleka mpunga hadi Amerika walipoulima katika koloni zao.

[hariri] Kilimo

Hadi leo maeneo makuu ya kilimo cha mpunga yako Asia hasa China, Bara Hindi na Asia ya Kusini-Mashariki. Asilimia 95 ya mavuno ya dunia hupatikana huko. Maeneo mengine ya maana ni kusini ya Marekani na Italia ya Kaskazini. Penginepo mavuno hayana maana ya kimataifa hata kama kilimo cha mpunga kwenye nchi kama Tanzania au Kenya ina umuhimu fulani wa kimahali.

Mpunga hulimwa hasa kwa njia mbili:

  • "bichi" kwenye mashamba yanayogharikishwa na mpunga unapandwa katika maji.
  • "kavu" kwenye mashamba ya kawaida kwa kutegemea mvua

Kwenye mtindo "bichi" mpunga hupandwa katika maji na mimea hukua kwenye maji vilevile. Maji huzuia majani ya kando yasiyotakiwa na wadudu wengi. Wakulima wengine wanatumia mabwawa yale pia kwa kukuza samaki kwenye shamba wakati wa mafuriko. Wakati wa kuiva maji huondolewa ili mpunga upate kukauka kabla ya mavuno.


[hariri] Viungo vya Nje

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: